
Didier Drogba akifunga goli
Goli moja la
Didier Drogba la dakika ya 45 lilitosha kuipatia ushindi timu ya Chelsea
almaarufu kama The blues watoto wa Darajani jijini London. Mechi ilikuwa ngumu
na ilitawaliwa kwa kiasi kikubwa na Barcelona kama ilivyo kawaida yao ya kupiga
pasi nyingi na kuwaacha Chelsea kuwa wakabaji muda wote.
Jitihada za
Barcelona kupata goli ziligonga mwamba kutokana na ubora wa safu ya ulinzi ya
Chelsea ambayo ilikuwa haipitiki kiurahisi huku golikipa wao Peter Cech akiwa
imara golini kuidaka michomo yote ya timu pinzani. Chelsea na Barcelona
wanasubiri kurudiana tena kipindi kijacho katika uwanja wa nyumbani wa
Barcelona wa Nou Camp.
Drogba akishangilia mara baada ya kufunga goli
Vikosi
Chelsea (4-3-3): Cech; Ivanovic, Cahill,Terry (c),
Cole; Lampard, Mikel, Meireles; Mata (Kalou 73), Drogba, Ramires
(Bosingwa 86).
Wachezaji wa akiba wasiotumika: Turnbull, Essien, Malouda, Torres, Sturridge.
Mfungaji: Drogba dk 45
Wachezaji wa akiba wasiotumika: Turnbull, Essien, Malouda, Torres, Sturridge.
Mfungaji: Drogba dk 45
Barcelona (4-3-3): Valdes; Alves, Puyol (c), Mascherano,
Adriano; Xavi (Cuenca 85), Busquets, Iniesta; Messi, Sanchez (Pedro 65),
Fabregas (Thiago 78).
Wachezaji wa akiba wasiotumika:: Pinto, Pique, Batra, Keita.
Wachezaji wa akiba wasiotumika:: Pinto, Pique, Batra, Keita.
Refarii: Felix
Brych
Watazamaji: 38,039
Watazamaji: 38,039
No comments:
Post a Comment