Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya kukabiliana na Uhalifu wa Kivita ameapishwa mjini Hague jana.
Bi Fatou Bensouda, aliyekuwa wakati mmoja Waziri
wa Haki nchini Gambia,ndiye Mwafrika na pia mwanamke wa kwanza
kushikilia cheo hicho.
Mojawapo
wa wajibu wake wa mwanzo ni kumleta Hague mwana wa aliyekuwa kiongozi
wa Libya, Muamar Gaddafi, Saif al-Islam Gadaffi, ambaye ameshtakiwa kwa
makosa dhidi ya binadamu na wakati huohuo kuongoza mashtaka
yanayomkabili aliyekuwa kiongozi wa Ivory Coast, Laurant Gbagbo.
Fatou Bensouda amechukua nafasi ya mtangulizi
wake aliyeondoka, Luis Moreno Ocampo, ambaye ameongoza mahakama hiyo kwa
zaidi ya mwongo mmoja.
Kesi ya rais wa zamani wa Liberia, Charles
Taylor, ilisikizwa na mahakama mahakama ya Umoja wa mataifa
inayosikiliza kesi za waliohusika na vita vya wenyewe kwa wenyewe
Sierra Leone.
Sierra Leone.
Bi Bensouda amekuwa akihudumu kama naibu wa Luis Moreno-Ocampo anayemaliza kazi yake katika mahakama ya ICC.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa licha ya kwamba Bi
Bensouda sio mgeni kwa mambo ya Hague, uteuzi wake unakuja wakati mfumo
wa sheria ya kimataifa unahojiwa sana.
Pia anachukua jukumu hilo wakati kuna mtafaruku
katika mahakama hiyo huku maafisa wanne wa mahakama hiyo wakiwa
wanazuiliwa nchini Libya.
Thomas Lubanga
Mwandishi wa BBC anasema kuwa Bi Bensouda anasifika kwa kuwa mtulivu kitu ambacho huenda kimemsaidia katika kazi yake.
Ikizingatiwa kuwa washukiwa wengi ambao kesi zao
ziko katika mahakama ya ICC ni waafrika na hili limekosolewa huku ofisi
ya mwendesha mkuu wa mashtaka ikisemekana kuwalenga zaidi waafrika.
Inatarajiwa kuwa kwa sababu Bi Bensouda mwenyewe
ni Mwafrika tena wakili, huenda akasaidiwa na hili kunyamazisha
wakosoaji wake, kulinagana na wadadisi.
Mwezi Machi mbabe wa kivita kutoka DRC, Thomas
Lubanga alipokea hukumu ya kwanza ya kesi yake ikiwa hukumu ya kwanza
kuwahi kutolewa na mahakama hiyo tangu kuundwa kwake miaka kumi
iliuopita.
Kikosi cha viongozi wa mashtaka wanataka Lubanga
apokee miaka 30 jela kwa makosa ya kutumia watoto kama wanajeshi wakati
wa vita mashariki mwa nchi yo kati ya mwaka 2002 na 2003.
No comments:
Post a Comment