
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla
akikabidhi kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mama wa marehemu Steven
Kanumba ikiwa ni rambirambi ya Serikali kwa familia.
James Magai na Nora Damian NDEREMO na vifijo vya wapenzi na Chadema, jana viliitikisa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam baada ya Jaji Upendo Msuya kutupilia mbali madai ya aliyekuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia CCM, Hawa Ngh’umbi kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, John Mnyika wa Chadema. Huu ni ushindi wa pili wa Mnyika dhidi ya Ngh’umbi baada ya kumshinda katika matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo la Ubungo, katika uchaguzi wa Oktoba 31, 2010. Katika hukumu hiyo ya kurasa 57 aliyoisoma kwa saa 1:21 (kuanzia saa 4:10 hadi 5:31), Jaji Msuya alitupilia mbali hoja zote tano, ambazo pande zote ziliyakubali kama mambo yaliyokuwa tata, hivyo kuhitaji uamuzi wa mahakama. Jaji Msuya alitupilia mbali madai yote ya Ngh’umbi akisema ameshindwa kuyathibitisha mahakamani pasi na shaka, huku akidai kuwa ushahidi wa shahidi wa kwanza (PW10 upande wa madai) ulikuwa ni maneno ya kusikia tu ambayo hakuyashuhudia. Ngh’umbi alifungua kesi dhidi ya Mnyika akidai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa taratibu wakati wa mchakato wa kampeni na utangazaji matokeo. Mbali na Mnyika ambaye alikuwa mdaiwa wa pili katika kesi hiyo wadaiwa wengine walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambaye ni mshtakiwa wa kwanza na Msimamizi wa Uchaguzi (Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni). Katika kesi hiyo namba 107 ya mwaka 2010, Ngh’umbi ambaye alikuwa akitetewa na Wakili Issa Maige, katika hati yake ya madai na wakati akitoa ushahidi wake mahakamani pamoja na mashahidi wake alidai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika uchaguzi huo. Ngh'umbi alidai kuwa, ukiukwaji wa sheria ulifanywa katika mchakato wa ujumlishaji wa kura na utangazaji wa matokeo, hivyo uliathiri matokeo ya uchaguzi huo kwa ujumla wake. Kutokana na madai hayo, Ngh'umbi aliiomba Mahakama pamoja na mambo mengine ibatilishe matokeo hayo na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo. Hata hivyo, katika hukumu yake Mahakama ilitupilia mbali madai na maombi yote ya Ngh’umbi na kumthibitisha Mnyika kuwa mbunge halali wa jimbo hilo. Katika hukumu hiyo, Jaji Msuya alisema upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi wachache na kwamba, mlalamikaji huyo alipaswa kuwaita mahakamani baadhi ya watu kutoka upande aliokuwa akiulalamikia kwenda kumtetea. Chadema walipuka Hukumu hiyo ya Jaji Msuya iliamsha shangwe kubwa, makofi na miluzi miongoni mwa wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika ndani na nje ya mahakama hiyo, wakifuatilia hukumu hiyo kupitia kwenye spika zilizowekwa nje ya ukumbi wa mahakama. Wakati Chadema wakichekelea, upande wa mlalamikaji Ngh’umbi na Wakili wake, Maige walielezea kutoridhishwa na hukumu hiyo huku wakielezea kushangazwa na sababu alizozitoa Jaji Msuya kutupilia mbali madai yao na kumpa ushindi Mnyika. Kwa upande wao wafuasi wa Chadema walielezea kuridhishwa na hukumu hiyo huku Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe ambaye pia alihudhuria mahakamani hapo akisema kuwa Mahakama imedhihirisha kuwa inatenda haki hata kwa wapinzani. Katika hukumu yake, Jaji Msuya alisema anatambua kuwa wingi wa mashahidi si kigezo cha kushinda kesi ila kuaminika na kukubalika kwa ushahidi wa mashahidi. Alisema mlalamikaji alishindwa kuithibitishia mahakama madai yake kwa kushindwa kuwaita mahakamani mashahidi wengi zaidi ili kuunga mkono ushahidi wa mashahidi wake wawili. Baadhi ya mashahidi ambao Jaji Msuya aliwataja kwamba walipaswa kuitwa mahakamani na upande wa walalamikaji ni pamoja na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Lambart Kyaro na aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Rajabu Kiravu. Kutokana na sababu hizo, Jaji Msuya alitupilia mbali madai yote ya Ngh’umbi akisema ameshindwa kuthibitisha madai yake katika hoja zote tano ambazo zilipaswa kutolewa uamuzi. Hoja ambazo Ngh’umbi alipaswa kuzithibitisha mahakamani ni pamoja na kama mlalamikiwa wa pili (Mnyika), alitoa kauli za kashfa dhidi yake, kwa kumwita fisadi akimtuhumu kuuza jengo la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na iwapo kulikuwa na upungufu katika ujazaji wa fomu namba 21B ( fomu za matokeo ya kura za ubunge vituoni). Hoja nyingine ni kama mlalamikiwa wa pili (Mnyika), aliingia na kompyuta (laptop) tano katika chumba cha majumuisho ya kura na kama ndizo zilizotumiwa na wasimamizi wa uchaguzi kuhesabu na kujumlishia kura pia kama Mnyika, aliingia na kundi la wafuasi wake katika chumba cha majumuisho kinyume cha sheria. Hoja ya mwisho ambayo Ngh’umbi alipaswa kuithibitisha ni kama kulikuwa na makosa katika ujazaji wa Fomu namba 24B (fomu za matokeo ya jumla ya ubunge) hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi mzima. Ushahidi Akitoa ushahidi wake mahakamani, Ngh’umbi alidai kuwa matokeo hayo siyo sahihi kwa sababu pamoja na mambo mengine, katika fomu ya matokeo yaliyotangazwa kuna kura 14,854, zisizojulikana mahali zilikotoka huku Ngh’umbi na shahidi wake wakiziita kura hewa. Alidai kuwa kwa mujibu wa fomu hiyo, kura halisi zilikuwa ni 119,823, kura halali zilikuwa ni 117,639 huku kura zilizokataliwa (zilizoharibika) zikiwa ni 2,184. Lakini, wakati wakijitetea, mdaiwa Mnyika alikanusha madai hayo yote licha ya kukiri kuwepo kwa mkanganyiko wa usahihi na uwiano wa kura katika Fomu namba 24B. Hata hivyo, alidai kuwa dosari hizo zinaweza kurekebishwa na kwamba haziathiri matokeo kiasi cha kuyafanya yawe batili. Mawakili wa utetezi, Justice Mulokozi kwa niaba ya AG na Edson Mbogoro kwa niaba ya Mnyika walidai kuwa mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha madai yake na hivyo, kuiomba mahakama iyatupile mbali. Hata hivyo, wakili wa Ngh’umbi, Issa Maige alitamba kuwa wameweza kuthibitisha madai yao kwa kiwango kinachohitajika kisheria na kuiomba mahakama itengue matokeo hayo yaliyompa ushindi Mnyika. Maige alisema madai mengine yameungwa mkono na mashahidi wa utetezi hususan DW1 aliyekiri Mnyika kuingia na kompyuta katika chumba cha majumuisho ingawa, alikanusha kuzitumia kufanyia majumuisho tofauti na Mnyika aliyekana kuingiza kompyuta hizo katika chumba hicho. Pia wakili Maige alihoji sababu ya mawakili wa serikali kutokuwaita mahakamani baadhi ya mashahidi ambao walitajwa na upande wa madai na wa wadaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine, katika mchakato wa uchaguzi huo. Wakili Maige aliwataja mashahidi hao ambao alidai walikuwa ni muhimu kuitwa mahakamani ili kujibu madai na kutoa ufafanuzi wa masuala yaliyowagusa kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mtaalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano wa Nec. Mkurugenzi huyo alidaiwa kwamba ndiye alikagua kompyuta zilizotumika kufanyia majumuisho ya kura badala ya zile zilizotoka Manispaa ya Kinondoni kutokana na mfumo wa awali ulioandaliwa na Nec kuonekana kuwa haufai. Maige alidai kuwa kitendo cha kushindwa kumwita mkurugenzi huyo mahakamani kutoa maelezo ya ukaguzi alioufanya na mbinu alizozitumia kuithibitishia mahakama kuwa katika kompyuta hizo isingewezekana kuingizwa taarifa za kughushi ni kinyume cha sheria. Akirejea kesi ya Stanbic Bank (T) Ltd dhidi ya Woods (T) Ltd namba 48 ya mwaka 2002, alidai Mahakama ilishatoa mwongozo kuwa ushahidi wa kitaalamu hauwezi kuthibitishwa kwa maneno matupu, pasipo mtaalamu kuitwa kuutolea ufafanuzi. Wakili Maige alidai kuwa upande wa madai umethibitisha kuwa kompyuta zisizostahili kisheria ndizo zilizotumika kufanya majumuisho na kwamba, ndizo zilizosababisha kuwepo kwa mkanganyiko uliojitokeza katika fomu ya matokeo wa kura zaidi ya 14,000 zisizo na maelezo. Hata hivyo, katika hukumu yake Jaji Msuya alisema jukumu la kuwaita mashahidi hao akiwemo mkurugenzi huyo na Kiravu lilikuwa ni la mlalamikaji na kwamba, kwa kushindwa kufanya hivyo ameshindwa kuthibitisha madai yake. Kuhusu makosa katika ujazaji wa fomu namba 24, Jaji Msuya alikubaliana na hoja za utetezi ni makosa ya kibinadamu akidai kuwa kulingana na mchakato wa jukumu hilo kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu ni jambo la kawaida kwa makosa kama hayo kutokea. “Katika hitimisho langu nakubali kuwa hakuna hoja hata moja katika hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho kama ilivyodaiwa kuthibitishwa,” alisema Jaji Msuya na kuongeza: “……ninatamka kuwa mdaiwa wa pili alichaguliwa kihalali kuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010 kwa kura 16, 198. Mdai atalipa gharama za uchaguzi”. Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 31, Novemba 2, 2010 Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru alimtangaza Mnyika kuwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho kwa kura 66,742 dhidi ya Ngh’umbi aliyepata kura 50,544 akimzidi Ngh’umbi kura 16,168. Hata hivyo, Ngh'umbi hakuridhika na matokeo hayo ndipo alipofungua kesi hiyo Mahakama Kuu kupitia kwa Wakili wake Issa Maige akiiomba mahakama hiyo itengue matokeo ya uchaguzi huo. HABARI KWA HISANI YA GAZETI MWANANCHI |
UPELELEZI
wa kesi ya muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu
anayekabiliwa na kesi ya mauaji bado haujakamilika. Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Lakini jana Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine. Hakimu Agustina Mmbando aliahirisha kesi hiyo na hadi June 4, 2012 itakapotajwa tena mahakamani hapo. Hata hivyo jana Mahakama ya Kisutu ilibidi itumie jalada la muda kwa kuwa jalada halisi la kesi hiyo limepelekwa Mahakama Kuu na hakimu Mmbando alisema kuwa bado halijarudi. Jalada hilo lilipelekwa Mahakama Kuu Ijumaa ya Mei 18 baada ya jopo la Mawakili wa mshtakiwa huyo kuwasilisha maombi huko juu ya uchunguzi kuhusiana na umri halali wa msanii huyo. Umri wa mshtakiwa huyo umezua utata kama ni mtoto au ni mtu mzima, jambo ambalo limewalazimu mawakili hao kuwasilisha maombi hayo ya uchunguzi wa umri wake Mahakama Kuu. Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo na Wakili Peter Kibatala Mei 15, 2012 na yamepangwa kusikilizwa na Jaji Dk Fauz Twaib Mei 28, 2012. Mawakili wa mshtakiwa huyo walifikia uamuzi wa kwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu baada ya kugonga mwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Kabla ya kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu, mawakili hao mawakili hao waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 7,2012 wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa bado ni mtoto. Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwamba kwa maana hiyo yeye bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima. Kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo wakili Kenedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18 kama inavyotamkwa mahakamani. Alidai kuwa hata cheti cha kuzaliwa walichokiwasilisha mahakamani kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa hivyo kuwa na umri wa miaka 17. “Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inatafsiri kuwa mtoto ni yule aliyekuwa na umri chini ya miaka 18 hivyo katika suala la mteja wetu alipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto,” alidai Wakili Fungamtama. Hata hivyo upande wa mashitaka kupitia kwa wakili Elizabeth Kaganda ulipinga maombi hayo na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na hivyo kuomba wapewe muda zaidi. |
Jana, Shonza akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, alilikana tamko la Heche wiki iliyoipita akisema hakuna kikao ambacho baraza hilo lilikaa na kutoa kauli moja kumjadili Shibuda. Hii ni mara ya tatu kwa Shibuda kusababisha mgongano ndani ya Chadema. Aliwahi kupinga msimamo wa kutotambua matokeo ya urais wa Jakaya Kikwete na badala yake, alishiriki tafrija Ikulu ndogo Chamwino, baada ya mkuu huyo wa nchi kuzindua Bunge la 10 na pia, aliwahi kupinga msimamo wa chama hicho kukataa posho bungeni badala yake alitaka ziongezwe hadi Sh500,000 huku akiziita ni, “ujira wa mwiha” na kuwarushia makombora baadhi ya viongozi wake akisema ni wabunge wafanyabiashara. Katika sakata hilo la sasa, Shonzi alisema: “Naomba ifahamike kwamba tamko alilolitoa Heche siyo la Baraza, bali ni lake kama Heche. Alipokuwa akitoa tamko hilo hakukuwa na kikao chochote cha Baraza cha viongozi wa kitaifa wala Sekretarieti ya Baraza la Vijana la Chadema ili kulijadili suala hili kwa kina bali, alitumia mwamvuli wa vijana kuhalalisha hoja yake.” Shonza alisema tamko alilolitoa dhidi ya Shibuda liliandaliwa na kuandikwa na Ofisa Habari wa Chadema Makao Makuu, kitu ambacho ni kinyume na utaratibu na kanuni za Bavicha. “Bavicha tumejikamilisha kwa maana ya kwamba, tuna uongozi wetu kamili wa taifa. Tuna ofisi zetu ambazo ni nje ya ofisi za makao makuu sasa iweje tamko hilo likaandaliwe makao makuu tena na mtu ambaye hahusiki na Bavicha?” Shonza alisema kama utaratibu huo alioutumia Heche ungekuwa unatumiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kufanya uamuzi binafsi pasipo kuyajadili na sekretarieti ya chama, wasingeweza kufikia matunda yanayoonekana hivi sasa. Msimamo wa Heche Wakati Makamu huyo akimrushia makombora bosi wake, jana Heche naye alitoa tamko akisema: “Natoa taarifa kwa umma kwamba baada ya mashauriano, Katibu wa Bavicha, Deogratias Siale ameitisha kikao cha sekretariati taifa Alhamisi, Mei 24, 2012, kwa ajili ya kujadili na kuwasilisha mapendekezo kwenye vikao halali vya chama kwa ajili ya hatua zaidi.” Aliongeza, “Wakati huohuo, nimejulishwa kuwa Makamu wangu (Shonza), leo amezungumza na vyombo vya habari na kukanusha taarifa niliyotoa kwa niaba ya Bavicha. Itambulike kuwa majukumu na mamlaka ya mwenyekiti na kiongozi mwingine yeyote wa Baraza yanabainishwa na Kanuni za Baraza letu kifungu 5.4.1, ambayo mwenyekiti ndiye msemaji mkuu wa Baraza na pia ndiye kiongozi mkuu wa Baraza katika ngazi husika.” Alisema kifungu cha 5.4.2 kinabainisha majukumu ya makamu mwenyekiti ambaye anapaswa kufanya kazi chini ya mwenyekiti na ndiye msaidizi wake. Alisema Katiba ya chama ambayo ndiyo msingi mama wa shughuli za Baraza katika kanuni zake kifungu cha 7.7.1, inabainisha kazi za mwenyekiti na pia anaweza kufanya nini na wakati gani kwa kushauriana na nani. “Kwa kutumia kifungu hiki, nilipokea ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Bavicha, akiwemo makamu mwenyekiti na kushauriana na Katibu na kuona haja ya kutoa kauli na mwongozo wa nini kitafuata kwa niaba ya baraza kama hatua ya kwanza,” alisema na kuongeza: Bavicha Shinyanga Bavicha Mkoa wa Shinyanga nalo jana limetoa tamko na kumkosoa Shibuda. Tamko hilo lililotolewa na Mwenyekiti wake, Nzemo Renatus, lilisema: “Tatizo letu na Shibuda ni kutoa kauli hii huku katiba ya Chadema na taratibu zake anazifahamu. Lakini mbaya zaidi anakidhalilisha chama kwa kutoa kauli nzito katika kikao cha mahasimu wetu wakuu wa kisiasa, CCM huku akiwa mwanachama wetu. Ni sawa na mvuvi anayetoboa mtumbwi wake mwenyewe akiwa katikati ya Ziwa au Bahari.” “Kwa niaba ya Bavicha Mkoa wa Shinyanga, naungana na kauli ya Mwenyekiti wa Bavicha Taifa. Tunaomba aitishe kamati ya utendaji ya Taifa haraka iwezekanavyo tuweze kupitisha maazimio ya kauli tatanishi za Mbunge Shibuda.” |
KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo hao wanamiliki mali na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi.Maofisa saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi. Tuhuma hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa kuanza kazi juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo itaanza rasmi kazi zake leo. Habari za uhakika kutoka ndani ya Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki akaunti ya fedha za kigeni. Kigogo huyo anahusishwa pia na mtandao wa utoaji vibali bandia kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi mkoani Kilimanjaro au kufanya kazi za kujitolea. Ripoti hiyo imetaja taasisi 13, zikiwamo zisizo za kiserikali (NGO), hospitali na hoteli za kitalii zinazodaiwa wageni wake walipewa vibali bandia. Mbali na kumhoji meneja huyo, inadaiwa pia walifanya mahojiano na uongozi wa kiwanda kimoja kinachodaiwa kukutwa na vibali bandia vya wageni 84. Taarifa hizo zilidai kuwa maofisa wengine waandamizi wa Uhamiaji kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam walitarajiwa kuwasili Moshi juzi kuungana na wenzao. Baadhi ya maofisa waliotajwa katika ripoti hiyo kwamba wana utajiri ni wale waliokumbwa na uhamisho katika idara hiyo, Kia miezi mitatu iliyopita. Katika ripoti hiyo, kigogo mmoja mwenye cheo cha DCI anadaiwa kukutwa na Sh700 milioni katika akaunti yake, achilia mbali kumiliki mali za mamilioni. Mbali na maofisa hao kumiliki mamilioni ya fedha taslimu, pia wanadaiwa ‘kufanya kufuru’ ya kununua magari ya kifahari, nyumba na viwanja. Ripoti hiyo inayodaiwa kuandikwa na Maofisa Uhamiaji wazalendo, imepinga hatua ya kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine, maofisa wanaotuhumiwa kukutwa na utajiri ambao haulingani na vipato vyao. “Tunataka ufanyike ukaguzi wa kina wa vibali vyote vilivyotolewa kati ya 2009/2010, 2010/2011 hadi 2012 na taasisi zote zionyeshe nakala za vibali,” imedai. Pia taarifa hiyo imependekeza wenzao wote wanaotuhumiwa kuwa na utajiri wa kutisha wachunguzwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). “Haikuwa sahihi kuwahamisha na kuishia hapo, walipaswa wapelekwe Takukuru wachunguzwe chanzo cha utajiri wao.” Pia wametaka kigogo anayemiliki akaunti ya Dola, achunguzwe ili kujua alikuwa akifanya biashara gani nje ya utumishi wa umma na kama alilipa kodi kiasi gani. Baadhi ya maofisa Uhamiaji wamependekeza kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo katika kipindi hiki kwa hofu ya kuingilia na kuvuruga uchunguzi. Wiki iliyopita, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Magnus Ulungi aliwaambia waandishi wa habari kuwa imeundwa kwa tume ya kumchunguza kigogo huyo. Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilisema tume hiyo imepanua wigo wa uchunguzi juu ya kuwapo kwa vibali bandia katika taasisi mbalimbali. Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Naodha alikaririwa akisema Kilimanjaro ni moja kati ya mikoa minane inayomtia kichefuchefu nchini. Waziri huyo alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na mtandao wa uingiaji wahamiaji haramu nchini pia kutoa vibali bandia kwa wageni. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipoulizwa juzi kuhusu sakata hilo alisema ni vyema Uhamiaji ikapewa nafasi ya kuchunguza suala hilo kwa kuwa tayari imeshateua tume ya uchunguzi. “Kamishna Mkuu wa Uhamiaji tayari amelifanyia kazi jambo hilo kwa uzito unaostahili. Tuwape nafasi walichunguze si vyema kuanza kuingilia katika hatua hii ya mwanzo,” alisema. Wahamiaji haramu Serikali, bila mafanikio, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukomesha tatizo la wahamiaji haramu linalotajwa kuwa chanzo cha utajiri wa baadhi ya vigogo wa Idara ya Uhamiaji. Miongoni mwa mikakati iliyowahi kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ni pamoja na idara hiyo kufanya utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe kubaini chanzo cha ongezeko la wahamiaji haramu nchini. Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni mwaka 2007/2008 , aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Joseph Mungai alisema matokeo ya utafiti huo ni kuisaidia Serikali kujua chanzo cha tatizo hilo na jinsi ya kupambana nalo kwa ufanisi zaidi. Hatua nyingine zinazochukuliwa ni pamoja na maofisa Uhamiaji kushiriki katika vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji, ili kuwapa wananchi elimu juu ya masuala yanayohusu uraia na jinsi ya kukabiliana na wahamiaji haramu; Kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari; Kuweka mtandao wa kompyuta katika vituo vyote vya Uhamiaji ili kuviunganisha na makao makuu. Pamoja na Serikali kutangaza mkakati huo miaka mitano iliyopita, wahamiaji haramu limeendelea kuwa tatizo sugu linalotia doa utendaji wa idara hiyo. HABARI KWA HISANI YA GAZETI MWANANCHI |
![]() |
Mmoja wa wanachama wa Yanga, anayeitwa Nyachia akionyesha kadi yake wakati wa kujisajili kuingia kwenye mkutano huo. |
PERSONAL SECRETARY - SOMANGA Qualification: Holder of form IV/VI certificate with Diploma in secretarial or full secretarial certificate Apply: Station Manager SomangaGas plant Tanesco Box 26 ,Kilwa Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 22, 2012 STOREMAN Qualification: Tertiary qualifications,valid Tanzania driving license will be added advantage Apply: buzrecruitment@barrick.com Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 20, 2012 SITE SERVICES MANAGER Qualification: Diploma or degree in hotel Management or food & beverage or recognition experience in catering and Accomodation Apply: buzrecruitment@barrick.com Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 20, 2012 COMMUNITY RELATIONS MANAGER Qualification: Bachelor degree in socilogy,economics,community development regional planning Apply: buzrecruitment@barrick.com Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 20, 2012 STORE KEEPER FOR - MOROGORO Qualification: College Diploma on sales and/or marketing Apply: Human Resources Manager Sao Hill Industry Limited Box 4730 , Dar es Salaam Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 25, 2012 SALES OFFICER - DODOMA Qualification: College Diploma on sales and/or marketing Apply: Human Resources Manager Sao Hill Industry Limited Box 4730 , Dar es Salaam Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 25, 2012 SALES OFFICER - MOROGORO Qualification: College Diploma on sales and/or marketing Apply: Human Resources Manager Sao Hill Industry Limited Box 4730 , Dar es Salaam Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 25, 2012 YARD MANAGER - MOROGORO Qualification: University Diploma om marketing or business administration Apply: Human Resources Manager Sao Hill Industry Limited Box 4730 , Dar es Salaam Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 25, 2012 QUALITY MANAGER Qualification: Advanced diploma or degree in food technology,laboratories(BLS)from recognized University or College Apply: Email ; recruitmentpowerfoods@gmail.com Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 22, 2012 LOGISTIC/WAREHOUSE OFFICER Qualification: A holder of Certificate of East Africa Customs, Clearing and freight forwading practices from TRA Tax Administration Apply: Email ; recruitmentpowerfoods@gmail.com Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 22, 2012 FINANCIAL COTROLLER Qualification: Bachelor of Commerce degree Accounting or MBA in Finance with mandatory professional qualification in the Accounting profession CPA(T) or equivalent Apply: email; recruitmentpowerfoods@gmail.com Details:Daily News May 08, 2012 Deadline: May 22, 2012 PERSONAL ASSISTANT MANAGEMENT Qualification: Advanced Secondary education and Diploma in Secretarial studies Apply: The Human Resources Manager, AccesBank Box 95061 ,Dar es salaam Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 23, 2012 BRANCH MANAGER - DAR ES SALAAM Qualification: Degree in Finance,Accountancy, Economics or equivalent full professional qualification in banking Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 TELEPHONE OPERATOR / RECEPTIONIST- UNGUJA Qualification: National form IV Certificate in Division III plus a certificate in front Office Management fro a recognized Institution Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 CREDIT OFFICER - UNGUJA Qualification: University degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 CREDIT OFFICER - PEMBA Qualification: University degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 AUDITOR - UNGUJA Qualification: University degree or Advanced Diploma in Accountancy,Finance,Banking ,Business Adminsistration or Computer Science or equivalent qualification Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 FINANCE OFFICER- 2 POSTS (UNGUJA) Qualification: Holder of degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 RISK AND COMPLIAANCE OFFICER - UNGUJA Qualification: Degree in Banking, Finance,Accounting or Business Administration, from recognized University or Institution Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 CUSTOMER SERVICES OFFICER (ISLAMIC BANKING) -DAR ES SALAAM Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 CUSTOMER SERVICES OFFICER ( ISLAMIC BANKING) - PEMBA Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 LEGAL OFFICER - UNGUJA Qualification: University degree in law with bias in Company and Commerical law Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 CUSTOMER SERVICES OFFICER - UNGUJA Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 BANK OPERATIONS OFFICER- UNGUJA Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 TELLER - 3 POSITIONS - PEMBA Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 TELLER - 2 POSITIONS - UNGUJA Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent Apply: The Managing Director The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd Box 1173 ,Zanzibar Details:Daily News May 11, 2012 Deadline: May 25, 2012 DEPUTY CHIEF FINANCIAL OFFICER Qualification: A holder of Master’s Degree either in Accounts, Finance,Economics,Public Finance or equivalent qualification Apply: Managing Director National Development Corporation Box 2669 ,Dar es Salaam Details:Daily News May 04, 2012 Deadline: June 05, 2012 DEPUTY CHIEF EXECUTIVE OFFICER Qualification: Post Graduate degree in Engineering,(Mechanical Electrical,Civil process,mining or geology),Economics or business Administration Apply: Managing Director National Development Corporation Box 2669 ,Dar es Salaam Details:Daily News May 04, 2012 Deadline: June 05, 2012 .hisani ya gazeti mwananchi |
Kwa mujibu wa maelezo ya FDA, mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU bila kutumia kondomu na hatomuambikiza. Matokeo ya utafiti huo yaliwahi kuchapishwa kwenye gazeti hili toleo la Februari 12, mwaka huu na sasa kilichofanyika ni FDA kuidhinisha Truvada ambayo ilionyesha kufanya kazi vizuri ikilinganishwa na ARV nyingine. Uidhinishaji wa dawa Jopo la wanasayansi 22 wa FDA waliokutana Jijini Washington wiki iliyopita, walipitisha Truvada baada ya kupitia ripoti ya utafiti kuhusiana na ufanyaji kazi wa dawa za ARV. Wanasayansi hao waliisifu dawa hiyo baada ya kuonekana kufanya kazi vizuri kwa watu waliopo kwenye hatari ya kuambukizana VVU kwa kasi zaidi. Kwa namna dawa hiyo inavyofanya kazi, mwathirika akiitumia hawezi tena kumwambukiza mtu mwingine ambaye atashiriki naye tendo la ndoa bila kutumia kondomu. Lakini, dawa hiyo masharti yake hayatofautiani na yale ya ARV kwani mtumiaji atapaswa kuitumia maisha yake yote ili kumwekea kinga asiwaambukize wengine na yeye aishi muda mrefu. Kulingana na ripoti ya utafiti uliofanyika Marekani, dawa hiyo ina uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU hadi asilimia 90.Hata hivyo, kwa watu ambao wamekuwa wakitumia dawa holela hasa za ARV, hali imekuwa tofauti kwani Truvada imeonekana ikifanya kazi kwa kiwango cha asilimia 44 tu. "Hii ni ishara kwamba kuna kundi la watu ambao dawa hiyo haitafanya kazi kikamilifu kutokana na mazingira ya matumizi ya dawa holela,"ilisema sehemu ya ripoti. Hata hivyo, wanasayansi wanasema tatizo hilo linafanyiwa uchunguzi ili kupata njia bora ya kukabiliana na tatizo hilo. Faida ya Truvada Wataalamu wameeleza kwamba itasaidia watu ambao wana VVU lakini, hawapendi kufanya tendo la ndoa kwa kutumia kondomu."Leo ni siku ya tukio la kuwasisimua wengi katika kuzuia maambukizi ya HIV,” alisema mmoja wa wataalamu kutoka Taasisi ya kujitolea kusaidia jamii ya Fenway, Dk Kenneth Mayer ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa FDA walioipitisha dawa hiyo. "Ingawa (Truvada) haikuweza kuonyesha uwezo wa asilimia 100 kuzuia maambukizi ya VVU, namna inavyofanya kazi itakuwa na matokeo mazuri ya kupambana na Ukimwi duniani,” alisema Dk Mayer. Tahadhari Hata hivyo, wataalamu hao walihimiza kuwepo kwa uchunguzi zaidi wa kitafiti ili kujua kama Truvada itafanya kazi vizuri duniani kote.Mtaalamu wa Dawa kutoka Taasisi ya Taifa ya Saratani nchini Marekani (NCI), Dk Lauren Wood alilalamika akisema kuwa utafiti huo haukuzingatia matatizo ya figo. Alisema matatizo ya figo yamekuwa yakijitokeza kwa waathirika wengi wa Ukimwi hasa barani Afrika."Mimi sikufurahishwa sana kwa sababu utafiti huu haukuzingatia maeneo ambayo watu wengi wako kwenye hatari ya maambukizi,” alisema Dk Wood. Lakini, alisema utafiti uliofanyika nchini Marekani umeonyesha wazi kwamba ni dawa inayoweza kupunguza kwa kiwango kikubwa kasi ya kusambaa kwa VVU. Wataalamu kadha nao walisema pamoja na Truvada kupitishwa na FDA, ni lazima maelezo ya kitaalamu yatolewe kwa madaktari ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi yake. Mabingwa hao walipendekeza kwamba, wanaotumia kabla ya kuruhusiwa kutembea na wenzi wao bila kondomu lazima wachunguzwe kitaalamu ili wajulikane kama dawa iyo imewakubali au la. Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Afya cha Cincinnati, Dk Judith Feinberg alikosoa ripoti ya uchunguzi akisema ilipaswa kwenda mbali zaidi katika kuchunguza madhara yanayoweza kujitokeza kwenye matumizi ya dawa hiyo.“Tusipokuwa makini katika hilo, tunaweza tukawa tumepitisha jambo ambalo litasababisha madhara zaidi kuliko faida,” alionya Dk Feinberg. Utafiti wa ARV Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins ni miongoni mwa wale ambao walifanya uchunguzi juu ya ARV, kuwa moja ya dawa zinazopunguza maambukizi ya VVU. Watafiti hao walibainisha kuwa wale wanaotumia ARV baada ya muda fulani, huweza kushiriki tendo la ndoa bila ya kutumia kondomu na mtu ambaye hana VVU na asimwambukize kwa asilimia 95. Mkuu wa Mtandao wa Maabara za Kuchunguza VVU katika chuo hicho, Profesa Susan Eshleman alisema kwenye ripoti ya ugunduzi huo, wamebaini dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa HIV, sasa zinaweza kutumika kama sehemu ya kuzuia maambukizi. Profesa Eshleman alisema kwamba, mwathirika wa VVU anayetumia ARV kikamilifu, anaweza kujamiiana na mtu ambaye hana virusi bila kondomu na asimwambukize. “Huu ni ugunduzi wa kustajabisha,” alisema Profesa Eshleman akifafanua: “Matokeo haya yameleta mapambazuko mapya katika sayansi ya kuzuia maambukizi na inawaweka watafiti kwenye mazingira mazuri zaidi ya kupata suluhisho la kukabiliana na maradhi haya.” Walivyogundua Profesa Eshleman anasema utafiti huo walioupa jina la HPTN 052, walifanya kupitia maeneo mbalimbali ya dunia. Kwenye ripoti hiyo ambayo pia ilichapishwa kwenye jarida maarufu la kisayansi linaloitwa Science, watafiti hao walisema mtu anapotumia ARV, hufikia wakati fulani wingi wa virusi mwilini hupotea kiasi kwamba anakuwa karibu sawa na yule ambaye hajaambukizwa. “Jambo la msingi katika utafiti huu ni kwamba dawa hizi za kurefusha maisha zinapotumiwa kikamilifu, hupunguza mzigo wa virusi mwilini kwa zaidi ya mara 200. Ni sawa na kusema inapunguza hadi kufikia karibu na sifuri,” inaeleza ripoti hiyo. Ni katika mazingira hayo, ripoti hiyo inasema kuwa damu ya mwathirika inakuwa haina virusi na hivyo uwezekano wa kumuambukiza mpenzi wake unakuwa haupo. Ripoti hiyo inaeleza kuwa ARV inafanya kazi mbili, kwanza kurefusha maisha ya mwathirika kwa kupunguza virusi mwilini na pili ni kumkinga asiambukize wengine. Sifa nyingine ya ARV, alisema ni kupunguza uwezekano wa waathirika kupata ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kutokana na kiwango cha kinga za mwili kuongezeka. HABARI KWA HISANI YA MCL |