
Mbunge wa Jimbo la Ubungo(CHADEMA)Mheshimiwa John Mnyika
--
Hukumu imepangwa kutolewa tarehe 24 Mei 2012;tumemaliza majumuisho ya
kesi dhidi yetu. Mawakili wote wawili wa upande wa utetezi wametimiza
wajibu wao. Pamoja na kuwa mawakili kwa ujumla walizungumza kwa zaidi ya
saa saba,namnukuu kiduchu Wakili wetu Mbogoro:“Mshindi wa uchaguzi
anatokana na maamuzi ya watu wengi,haki ambayo huipata kwa nadra kila
baada ya miaka mitano na ni mchakato unaotumia fedha nyingi za walipa
kodi.Hivyo kiwango cha uthibitisho wa madai yoyote lazima kiwe bila ya
shaka yoyote…mlalamikaji Hawa Ng’umbi amesema mwenyewe mahakamani kuwa
hana tatizo na matokeo ya toka vituoni, malalamiko yake sio juu ya nani
mshindi.
Kwa kawaida kesi za uchaguzi hufunguliwa na wenye kupinga
ushindi wanaodai kuwa wangeshinda wao iwapo sheria zisingekiukwa; kama
hapingi matokeo ya vituoni ambayo majumuisho yake ndio yamempa Mnyika
ushindi; tunaweza kujiuliza tuko hapa kwa ajili gani?” Tuungane pamoja
katika sala na swala kumwombea kwa Mwenyezi Mungu Jaji Upendo Msuya
afanye maamuzi ya haki.
John Mnyika
Mbunge Jimbo la Ubungo(CHADEMA)-KWA NIABA YA HAKI NGOWI
No comments:
Post a Comment