Thursday, May 17, 2012

TCRA YATOA MAFUNZO JUU YA UMUHIMU WA KUTUMIA KOMPYUTA NA MFUMO WA DIGITALI


Katibu mkuu wa wizara ya Mawasiliano  Sayansi na Teknolojia Dr Florens Turuka akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kuelekea kilele cha siku ya sherehe ya mawasiliano duniani ambapo maadhimisho hayo yanatarajiawa kufanyika kesho Duniani kote, Dk Turuka amewaomba wafanya biashara wauze televisheni ambazo zipo katika mfumo wa Digital. Warsha hiyo imeanza leo hii katika Ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Prof, John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari  leo hii jijini Dar es Salaam kwenye Semina inayoambatana na Sherehe ya  siku ya mawasiliano Duniani. ambapo amewataka watanzania kuelewa umuhimu wa mawasiliano ya mtandao.
Baadhi ya wadau mblimbali wa mawasiliano nchini waliohudhuria kwenye warsha hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na watoa mada.
Mwanafunzi wa shule ya Msingi  Mapinduzi Zuwena Muddy, akitoa mafunzo ya namna ya kutumia Computer  kwa wadau waliohudhuria kwenye semina hiyo.
Mwanafunzi Jackson Joseph kutoka shule ya Msingi  Mapinduzi jijini Dar es Salaam manispaa ya Ilala, akihojiwa na waandishi wa habari juu ya faida ya matumizi  ya Computer.
Mwanafunzi Zuwena Muddy akisisitiza jambo katika mafunzo hayo kwenye warsha hiyo.

No comments:

Post a Comment