Saturday, May 26, 2012

Wabunge Wa Chadema Peter Msigwa na Joshua Nassari Nao Watua Washington DC

 Safari na muziki wameruka na wametua kwa salama na amani, wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kwanza kulia, Nassari Joshua, Dogo Janja akiwa na  Mhe.   Peter Msigwa ndani ya Washington DC
Wanachama wa Chadema Washington DC Anko Ludigo akiwa na Mhe Dogo Janja, Mkereketwa Libe aka Mwangombe, pamoja na Mhe. Peter Msigwa, wakiwa wameshikilia kadi za Chadema ambazo zipo tayari kwa kila  mwenye kupenda mabadiliko ya Tanzania.
--
Ndani ya jiji la Washington Dc Wabunge  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)   waibuka jijini hapa kwa vishindo, huku Watanzania mbali mbali waishio nchini Marekani wakiwasuburi kwahamu siku hiyo ya Jumapili Mei 27, 2012,

Madhumuni ya mkutano huo ni kukutana na Watanzania wanaoishi Nchini Marekani kuzungumza juu ya mpango mzima  wa maendeleo  ya nchi yetu kwa jumla, mkutano huo utahudhuriwa na Mhe. Leticia  Nyerere, Mhe. Zitto Kabwe, Mhe. Nassari Joshua Marufu Dogo Janja na Mhe. Mchungaji Msigwa.

No comments:

Post a Comment