Thursday, May 31, 2012

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla Akabidhi Shilingi Milioni Kumi Kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba Kwa Niaba Ya Serikali.

 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mama wa marehemu Steven Kanumba ikiwa ni rambirambi ya Serikali kwa familia.

Monday, May 28, 2012

UAMSHO WAKANA KUHUSIKA NA VURUGU ZANZIBAR

THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION

P. O. BOX: 1266
Tel: +255-777-419473 / 434145-
FAX +255-024-2250022
E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR

Tarehe 27MAY2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee
Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika
Uislamu.

Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na
Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya
uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama
alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu
kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila
kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na
likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu
unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala
zisiharibiwe.

Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea
kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali,
mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani
kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu.
Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na
yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale
wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya
na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi
zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa
Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya
dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia
haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya
kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na
utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil
ya kulinda haki za wengine.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na
kutetea haki za binadamu kwa watu wote.

WABILLLAH TAWFIQ

Mlipuko mkubwa watokea jijini Nairobi

Mlipuko watokea Nairobi, Kenya na kujeruhi watu kadhaa.
Mlipuko umetokea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku majengo majengo yakiwa yanawaka moto.
Mlipuko huo umetokea ktika jengo lenye maduka madogo madogo mengi. Mwandishi wa BBC anasema mlipuko huo umesababisha bidhaa mbali mbali kama viatu, nguo na vioo vilivyovunjika kusambaa sehemu yote ya eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Kevin Mwachiro anasema Polisi wamelizungushia eneo hilo uzio wa utepe kwa ajili ya usalama. Ni mapema kutaja idadi ya majeruhi lakini vyombo vingine vya habari vinasema zaidi ya watu 28 wamejeruhiwa na mlipuko huo
Picha za Televisheni nchini humo zimeonyesha watu wakikimbia mbali na majengo yaliyo karibu katikati ya mji wa Nairobi.
Kamishna wa Polisi nchini Kenya Mathew Iteere, anasema huenda "hitilafu ya umeme" ndio chanzo cha mlipuko huo, kwa mujibu wa Televisheni ya NTV. Hata hivyo mlipuko huo unaiweka Nairobi katika hali ya wasiwasi.
Kumekuwa na milipuko kadhaa hivi karibuni ndani na nje ya mji huo mkuu huku baadhi ikihusishwa na kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab.
Timu ya waokoaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu imetumwa katika eneo la tukio kwenye mtaa huo wa Moi. Mtaa huo ni barabara kuu ambayo wakati wa mchana huwa na watu wengi, Shirika la habari la AP linasema.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia kulikuwa na mlipuko mkubwa na huku vipande vipande vya vioo na vitu vingine vikiwarukia na kujeruhi watu waliokuwa karibu, Gazeti la Nation linaripoti.
Gazeti hilo linaongeza kuwa mlipuko huo umetikisa majengo yaliyo karibu na harakati za kuwahamisha watu zimeanza. CHANZO BBC SWAHILI

Saturday, May 26, 2012

SOMA HII STORI YA HUYU JAMAA

JAMAA MMOJA NCHINI MAREKANI DESMOND HATCHET ANA KABILIWA NA KOSA LA KUSHINDWA KUTUNZA WATOTO WAKE 30 ALIOZAA NA WANAWAKE 11 TOFAUTI,JAMAA HUYO MWENYE UMRI WA MIAKA 33 ANAYETOKEA TENNESSEE,AMEIOMBA MAHAKAMA IWEZE KUMSAIDIA KULEA WATOTO WAKE KWA KUWA KIPATO CHAKE HAKIJITOSHELEZI.

Wabunge Wa Chadema Peter Msigwa na Joshua Nassari Nao Watua Washington DC

 Safari na muziki wameruka na wametua kwa salama na amani, wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kwanza kulia, Nassari Joshua, Dogo Janja akiwa na  Mhe.   Peter Msigwa ndani ya Washington DC
Wanachama wa Chadema Washington DC Anko Ludigo akiwa na Mhe Dogo Janja, Mkereketwa Libe aka Mwangombe, pamoja na Mhe. Peter Msigwa, wakiwa wameshikilia kadi za Chadema ambazo zipo tayari kwa kila  mwenye kupenda mabadiliko ya Tanzania.
--
Ndani ya jiji la Washington Dc Wabunge  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)   waibuka jijini hapa kwa vishindo, huku Watanzania mbali mbali waishio nchini Marekani wakiwasuburi kwahamu siku hiyo ya Jumapili Mei 27, 2012,

Madhumuni ya mkutano huo ni kukutana na Watanzania wanaoishi Nchini Marekani kuzungumza juu ya mpango mzima  wa maendeleo  ya nchi yetu kwa jumla, mkutano huo utahudhuriwa na Mhe. Leticia  Nyerere, Mhe. Zitto Kabwe, Mhe. Nassari Joshua Marufu Dogo Janja na Mhe. Mchungaji Msigwa.

Friday, May 25, 2012

ANGALIA: Mnyika afunika Dar




Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika akiwa amebebwa na Wafuasi wake baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kumtangaza jana kuwa mshindi halali katika matokeo yaliyompa ushindi katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010. Picha na Fidelis Felix
AMBWAGA TENA MGOMBEA CCM, MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MADAI YA NGH'UMBI
James Magai na Nora Damian
NDEREMO na vifijo vya wapenzi na Chadema, jana viliitikisa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam baada ya Jaji Upendo Msuya kutupilia mbali madai ya aliyekuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Ubungo kupitia CCM, Hawa Ngh’umbi kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, John Mnyika wa Chadema.

Huu ni ushindi wa pili wa Mnyika dhidi ya Ngh’umbi baada ya kumshinda katika matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo la Ubungo, katika uchaguzi wa Oktoba 31, 2010.

Katika hukumu hiyo ya kurasa 57 aliyoisoma kwa saa 1:21 (kuanzia saa 4:10 hadi 5:31), Jaji Msuya alitupilia mbali hoja zote tano, ambazo pande zote ziliyakubali kama mambo yaliyokuwa tata, hivyo kuhitaji uamuzi  wa mahakama.

Jaji Msuya alitupilia mbali madai yote ya Ngh’umbi akisema ameshindwa kuyathibitisha mahakamani pasi na shaka, huku akidai kuwa ushahidi wa  shahidi wa kwanza (PW10 upande wa madai) ulikuwa ni maneno ya kusikia tu ambayo hakuyashuhudia.

Ngh’umbi alifungua kesi dhidi ya Mnyika akidai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na ukiukwaji wa taratibu wakati wa mchakato wa kampeni na utangazaji matokeo.

Mbali na Mnyika ambaye alikuwa mdaiwa wa pili katika kesi hiyo wadaiwa  wengine walikuwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambaye ni mshtakiwa wa kwanza na Msimamizi wa Uchaguzi (Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni).

Katika kesi hiyo namba 107 ya mwaka 2010, Ngh’umbi ambaye alikuwa akitetewa na Wakili Issa Maige, katika hati yake ya madai na wakati akitoa ushahidi wake mahakamani pamoja na mashahidi wake alidai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa sheria katika uchaguzi huo.

Ngh'umbi alidai kuwa, ukiukwaji wa sheria ulifanywa katika mchakato wa ujumlishaji wa kura na utangazaji wa matokeo, hivyo uliathiri matokeo ya uchaguzi huo kwa ujumla wake.

Kutokana na madai hayo, Ngh'umbi aliiomba Mahakama pamoja na mambo mengine ibatilishe matokeo hayo na kuamuru ufanyike uchaguzi mdogo.

Hata hivyo, katika hukumu yake Mahakama ilitupilia mbali madai na maombi yote ya Ngh’umbi na kumthibitisha Mnyika kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Katika hukumu hiyo, Jaji Msuya alisema upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi wachache na kwamba, mlalamikaji huyo alipaswa kuwaita mahakamani baadhi ya watu kutoka upande aliokuwa akiulalamikia kwenda kumtetea.

Chadema walipuka
Hukumu hiyo ya Jaji Msuya iliamsha shangwe kubwa, makofi na miluzi miongoni mwa wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika ndani na nje ya mahakama hiyo, wakifuatilia hukumu hiyo kupitia kwenye spika zilizowekwa nje ya ukumbi wa mahakama.

Wakati Chadema wakichekelea, upande wa mlalamikaji Ngh’umbi na Wakili wake, Maige walielezea kutoridhishwa na hukumu hiyo huku wakielezea kushangazwa na sababu alizozitoa Jaji Msuya kutupilia mbali madai yao na kumpa ushindi Mnyika.

Kwa upande wao wafuasi wa Chadema walielezea kuridhishwa na hukumu hiyo huku Mwenyekiti wake wa Taifa, Freeman Mbowe ambaye pia  alihudhuria mahakamani hapo akisema kuwa Mahakama imedhihirisha kuwa inatenda haki hata kwa wapinzani.

Katika hukumu yake, Jaji Msuya alisema  anatambua kuwa wingi wa mashahidi si kigezo cha kushinda kesi ila kuaminika na kukubalika kwa ushahidi wa mashahidi.

Alisema mlalamikaji alishindwa kuithibitishia mahakama madai yake kwa kushindwa kuwaita mahakamani mashahidi wengi zaidi ili kuunga mkono ushahidi wa mashahidi wake wawili.

Baadhi ya mashahidi ambao Jaji Msuya aliwataja kwamba walipaswa kuitwa  mahakamani na upande wa walalamikaji ni pamoja na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Lambart Kyaro na aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Rajabu Kiravu.

Kutokana na sababu hizo, Jaji Msuya alitupilia mbali madai yote ya Ngh’umbi akisema ameshindwa kuthibitisha madai yake katika hoja zote tano ambazo zilipaswa kutolewa uamuzi.

Hoja ambazo Ngh’umbi alipaswa kuzithibitisha mahakamani ni pamoja na kama mlalamikiwa wa pili (Mnyika), alitoa kauli za kashfa dhidi yake, kwa kumwita fisadi akimtuhumu kuuza jengo la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na iwapo kulikuwa na upungufu katika ujazaji wa fomu namba 21B ( fomu za matokeo ya kura za ubunge vituoni).

Hoja nyingine ni kama mlalamikiwa wa pili (Mnyika), aliingia na kompyuta (laptop) tano katika chumba cha majumuisho ya kura na kama ndizo zilizotumiwa na wasimamizi wa uchaguzi kuhesabu na kujumlishia kura pia kama Mnyika, aliingia na kundi la wafuasi wake katika chumba cha majumuisho kinyume cha sheria.

Hoja ya mwisho ambayo Ngh’umbi alipaswa kuithibitisha ni kama kulikuwa na makosa katika ujazaji wa Fomu namba 24B (fomu za matokeo ya jumla ya ubunge) hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi mzima.

Ushahidi
Akitoa ushahidi wake mahakamani, Ngh’umbi alidai kuwa matokeo hayo siyo sahihi kwa sababu pamoja na mambo mengine, katika fomu ya matokeo yaliyotangazwa kuna kura 14,854, zisizojulikana mahali zilikotoka huku Ngh’umbi na shahidi wake wakiziita kura hewa.

Alidai kuwa kwa mujibu wa fomu hiyo, kura halisi zilikuwa ni 119,823, kura halali zilikuwa ni 117,639 huku kura zilizokataliwa (zilizoharibika) zikiwa ni 2,184.

Lakini, wakati wakijitetea, mdaiwa Mnyika alikanusha madai hayo yote licha ya kukiri kuwepo kwa mkanganyiko wa usahihi na uwiano wa kura katika Fomu namba 24B. Hata hivyo, alidai kuwa dosari hizo zinaweza kurekebishwa na kwamba haziathiri matokeo kiasi cha kuyafanya yawe batili.

Mawakili wa utetezi, Justice Mulokozi kwa niaba ya AG na Edson Mbogoro kwa niaba ya Mnyika walidai kuwa mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha madai yake na hivyo, kuiomba mahakama iyatupile mbali.

Hata hivyo, wakili wa Ngh’umbi, Issa Maige alitamba kuwa wameweza kuthibitisha madai yao kwa kiwango kinachohitajika kisheria na kuiomba mahakama itengue matokeo hayo yaliyompa ushindi Mnyika.

Maige alisema madai mengine yameungwa mkono na mashahidi wa utetezi hususan DW1 aliyekiri Mnyika kuingia na kompyuta katika chumba cha majumuisho ingawa, alikanusha kuzitumia kufanyia majumuisho tofauti na Mnyika aliyekana kuingiza kompyuta hizo katika chumba hicho.

Pia wakili Maige alihoji sababu ya mawakili wa serikali kutokuwaita mahakamani baadhi ya mashahidi ambao walitajwa na upande wa madai na wa wadaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine, katika mchakato wa uchaguzi huo.

Wakili Maige aliwataja mashahidi hao ambao alidai walikuwa ni muhimu kuitwa mahakamani ili kujibu madai na kutoa ufafanuzi wa masuala yaliyowagusa kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mtaalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano wa Nec.

Mkurugenzi huyo alidaiwa kwamba ndiye alikagua kompyuta zilizotumika kufanyia majumuisho ya kura badala ya zile zilizotoka Manispaa ya Kinondoni kutokana na mfumo wa awali ulioandaliwa na Nec kuonekana kuwa haufai.

Maige alidai kuwa kitendo cha kushindwa kumwita mkurugenzi huyo mahakamani kutoa maelezo ya ukaguzi alioufanya na mbinu alizozitumia kuithibitishia mahakama kuwa katika kompyuta hizo isingewezekana kuingizwa taarifa za kughushi ni kinyume cha sheria.

Akirejea kesi ya Stanbic Bank (T) Ltd dhidi ya Woods (T) Ltd namba 48 ya mwaka 2002, alidai  Mahakama ilishatoa mwongozo kuwa ushahidi wa kitaalamu hauwezi kuthibitishwa kwa maneno matupu, pasipo mtaalamu kuitwa kuutolea ufafanuzi.

Wakili Maige alidai kuwa upande wa madai umethibitisha kuwa kompyuta zisizostahili kisheria ndizo zilizotumika kufanya majumuisho na kwamba, ndizo zilizosababisha kuwepo kwa mkanganyiko uliojitokeza katika fomu ya matokeo wa kura zaidi ya 14,000 zisizo na maelezo.

Hata hivyo, katika hukumu yake Jaji Msuya alisema jukumu la kuwaita mashahidi hao akiwemo mkurugenzi huyo na Kiravu lilikuwa ni la mlalamikaji na kwamba, kwa kushindwa kufanya hivyo ameshindwa kuthibitisha madai yake.

Kuhusu makosa katika ujazaji wa fomu namba 24, Jaji Msuya alikubaliana na hoja za utetezi  ni makosa ya kibinadamu akidai kuwa kulingana na mchakato wa jukumu hilo kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu ni jambo la kawaida kwa makosa kama hayo kutokea.

“Katika hitimisho langu nakubali kuwa hakuna hoja hata moja katika hati ya madai iliyofanyiwa marekebisho kama ilivyodaiwa kuthibitishwa,” alisema Jaji Msuya na kuongeza:

“……ninatamka kuwa mdaiwa wa pili alichaguliwa kihalali kuwa mbunge wa Jimbo la Ubungo, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, 2010 kwa kura 16, 198. Mdai atalipa gharama za uchaguzi”.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 31, Novemba 2, 2010 Msimamizi wa Uchaguzi, Raphael Ndunguru  alimtangaza Mnyika kuwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho kwa kura 66,742 dhidi ya Ngh’umbi aliyepata kura 50,544 akimzidi Ngh’umbi kura 16,168.

Hata hivyo, Ngh'umbi hakuridhika na matokeo hayo ndipo alipofungua kesi hiyo Mahakama Kuu kupitia kwa Wakili wake Issa Maige akiiomba mahakama hiyo itengue matokeo ya uchaguzi huo. HABARI KWA HISANI YA GAZETI MWANANCHI

Thursday, May 24, 2012

Picha ya Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)Mheshimiwa John Mnyika baada Ya Kuibuka Kidedea Kwenye Kesi Ya Uchaguzi

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake katika Jimbo la Ubungo katika uchaguzi wa mwaka 2010, hukumu iliyotolewa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Pichani wafuasi wa Chadema wakiwa wamembeba juu kwa juu mara baada ya kutangazwa mshindi.

Tuesday, May 22, 2012

Upelelezi kesi ya Lulu ‘bado mbichi’


UPELELEZI wa kesi ya muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na  kesi ya mauaji bado haujakamilika.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Lakini jana Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine.
Hakimu Agustina Mmbando aliahirisha kesi hiyo na hadi June 4, 2012 itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Hata hivyo jana Mahakama ya Kisutu ilibidi itumie jalada la muda kwa kuwa jalada halisi la kesi hiyo limepelekwa Mahakama Kuu na hakimu Mmbando alisema kuwa bado halijarudi.

Jalada hilo lilipelekwa Mahakama Kuu Ijumaa ya Mei 18 baada ya jopo la Mawakili wa mshtakiwa  huyo kuwasilisha maombi huko juu ya uchunguzi kuhusiana na umri halali wa msanii huyo.

Umri wa mshtakiwa huyo umezua utata kama ni mtoto au ni mtu mzima, jambo ambalo limewalazimu mawakili hao kuwasilisha maombi hayo ya uchunguzi wa umri wake Mahakama Kuu.
Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo  na Wakili Peter Kibatala Mei 15, 2012 na yamepangwa kusikilizwa  na Jaji Dk Fauz Twaib Mei 28, 2012.

Mawakili wa mshtakiwa huyo walifikia uamuzi wa kwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu baada ya kugonga mwamba Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kabla ya kuwasilisha maombi hayo Mahakama Kuu, mawakili hao mawakili hao waliwasilisha maombi  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 7,2012  wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto wakidai kuwa bado ni mtoto.

Mawakili hao walidai mahakamani hapo kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na kwamba kwa maana hiyo yeye bado ni mtoto na kesi yake haipaswi kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.
Kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea msanii huyo wakili Kenedy Fungamtama alidai kuwa mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18 kama inavyotamkwa mahakamani.

Alidai kuwa hata cheti cha kuzaliwa walichokiwasilisha mahakamani kinaonyesha mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa hivyo kuwa na umri wa miaka 17.

“Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 inatafsiri kuwa mtoto ni yule aliyekuwa na umri chini ya miaka 18 hivyo katika suala la mteja wetu alipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto,” alidai Wakili Fungamtama.

Hata hivyo upande wa mashitaka kupitia kwa wakili Elizabeth Kaganda ulipinga maombi hayo na kudai kuwa bado wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na hivyo kuomba wapewe muda zaidi.

Monday, May 21, 2012

Vijana Chadema kwachafuka



Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), Joliana Shonza.
SAKATA la Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda kutangaza nia ya kuwania urais ndani ya Kikao cha Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM, sasa linaitikisa Chadema baada ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), Joliana Shonza kupingana hadharani na bosi wake, John Heche. Wakati Heche akiwa tayari ametoa tamko kumshambulia Shibuda akisema chama hicho hakitaruhusu mgombea wake urais  atangaze nia kwenye vikao vya CCM, Shonza ameibuka na kusema tamko hilo la bosi wake siyo la Bavicha ila ni lake binafsi.
Jana, Shonza akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, alilikana tamko la Heche wiki iliyoipita akisema hakuna kikao ambacho baraza hilo lilikaa na kutoa kauli moja kumjadili Shibuda.
Hii ni mara ya tatu kwa Shibuda kusababisha mgongano ndani ya Chadema. Aliwahi kupinga msimamo wa kutotambua matokeo ya urais wa Jakaya Kikwete na badala yake, alishiriki tafrija Ikulu ndogo Chamwino, baada ya mkuu huyo wa nchi kuzindua Bunge la 10 na pia, aliwahi kupinga msimamo wa chama hicho kukataa posho bungeni badala yake alitaka ziongezwe hadi Sh500,000 huku akiziita ni, “ujira wa mwiha” na kuwarushia makombora baadhi ya viongozi wake akisema ni wabunge wafanyabiashara. 
Katika sakata hilo la sasa, Shonzi alisema: “Naomba ifahamike kwamba tamko alilolitoa Heche siyo la Baraza, bali ni lake kama Heche. Alipokuwa akitoa tamko hilo hakukuwa na kikao chochote cha Baraza cha viongozi wa kitaifa wala Sekretarieti ya Baraza la Vijana la Chadema ili kulijadili suala hili kwa kina bali, alitumia mwamvuli wa vijana kuhalalisha hoja yake.”
Shonza alisema tamko alilolitoa dhidi ya Shibuda liliandaliwa na kuandikwa na Ofisa Habari wa Chadema Makao Makuu,  kitu ambacho ni kinyume na utaratibu na kanuni za Bavicha.
“Bavicha tumejikamilisha kwa maana ya kwamba, tuna uongozi wetu kamili wa taifa. Tuna ofisi zetu ambazo ni nje ya ofisi za makao makuu sasa iweje tamko hilo likaandaliwe makao makuu tena na mtu ambaye hahusiki na Bavicha?”
Shonza alisema kama utaratibu huo alioutumia Heche ungekuwa unatumiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kufanya uamuzi binafsi  pasipo kuyajadili na sekretarieti ya chama, wasingeweza kufikia matunda yanayoonekana hivi sasa.
Msimamo wa Heche
Wakati Makamu huyo akimrushia makombora bosi wake, jana Heche naye alitoa tamko akisema: “Natoa taarifa kwa umma kwamba baada ya mashauriano, Katibu wa Bavicha, Deogratias Siale ameitisha kikao cha sekretariati taifa Alhamisi, Mei 24, 2012, kwa ajili ya kujadili na kuwasilisha mapendekezo kwenye vikao halali vya chama kwa ajili ya hatua zaidi.”
Aliongeza, “Wakati huohuo, nimejulishwa kuwa Makamu wangu (Shonza), leo amezungumza na vyombo vya habari na kukanusha taarifa niliyotoa kwa niaba ya Bavicha. Itambulike kuwa majukumu na mamlaka ya mwenyekiti na kiongozi mwingine yeyote wa Baraza yanabainishwa na Kanuni za Baraza letu kifungu 5.4.1, ambayo mwenyekiti ndiye msemaji mkuu wa Baraza na pia ndiye kiongozi mkuu wa Baraza katika ngazi husika.”
Alisema kifungu cha 5.4.2 kinabainisha majukumu ya makamu mwenyekiti ambaye anapaswa kufanya kazi chini ya mwenyekiti na ndiye msaidizi wake.
Alisema Katiba ya chama ambayo ndiyo msingi mama wa shughuli za Baraza katika kanuni zake kifungu cha 7.7.1, inabainisha kazi za mwenyekiti na pia anaweza kufanya nini na wakati gani kwa kushauriana na nani.
“Kwa kutumia kifungu hiki, nilipokea ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Bavicha, akiwemo makamu mwenyekiti na kushauriana na Katibu na kuona haja ya kutoa kauli na mwongozo wa nini kitafuata kwa niaba ya baraza kama hatua ya kwanza,” alisema na kuongeza:
Bavicha Shinyanga
Bavicha Mkoa wa Shinyanga nalo jana limetoa tamko na kumkosoa Shibuda. Tamko hilo lililotolewa na Mwenyekiti wake, Nzemo Renatus, lilisema: “Tatizo letu na Shibuda ni kutoa kauli hii huku katiba ya Chadema na taratibu zake anazifahamu.
Lakini mbaya zaidi anakidhalilisha chama kwa kutoa kauli nzito katika kikao cha mahasimu wetu wakuu wa kisiasa,  CCM huku akiwa mwanachama wetu. Ni sawa na mvuvi anayetoboa mtumbwi wake mwenyewe akiwa katikati ya Ziwa au Bahari.”
 “Kwa niaba ya Bavicha Mkoa wa Shinyanga, naungana na kauli ya Mwenyekiti wa Bavicha Taifa. Tunaomba aitishe kamati ya utendaji ya Taifa haraka iwezekanavyo tuweze kupitisha maazimio ya kauli tatanishi za Mbunge Shibuda.”

Vigogo Uhamiaji wana utajiri wa kutisha



Rais Jakaya Kikwete akifafanua jambo siku zilizopita.
TUME YA KUWACHUNGUZA YAANZA KAZI LEO, WAHAMISHIWA MIKOANI KIAINA

KASHFA nyingine imeibuliwa katika Idara ya Uhamiaji.Taarifa mpya yenye kurasa tano, imewataja vigogo hao saba wakidaiwa kuwa na utajiri wa kutisha.Taarifa hiyo ambayo tunayo nakala yake, imedai kuwa vigogo hao wanamiliki mali na mamilioni ya shilingi katika akaunti zao binafsi.Maofisa saba wametajwa kwa majina na vituo vyao vya kazi ambavyo ni Lindi, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na Moshi.
Tuhuma hizo zimekuja wakati Tume Maalumu iliyoundwa kuchunguza tuhuma za ufisadi na utoaji wa vibali bandia kwa wageni, ikitajwa kuanza kazi juzi. Hata hivyo, habari kutoka wizarani zinaeleza kuwa timu hiyo itaanza rasmi kazi zake leo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Uhamiaji, zimedai kuwa baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wamemhoji meneja wa benki moja kubwa ya Moshi ili kupata ukweli wa madai kuwa kigogo mmoja wa Uhamiaji mwenye cheo cha Naibu Kamishna (DCI), anamiliki akaunti ya fedha za kigeni.
Kigogo huyo anahusishwa pia na mtandao wa utoaji vibali bandia kwa raia wa kigeni wanaofanya kazi mkoani Kilimanjaro au kufanya kazi za kujitolea.
Ripoti hiyo imetaja taasisi 13, zikiwamo zisizo za kiserikali (NGO), hospitali na hoteli za kitalii zinazodaiwa wageni wake walipewa vibali bandia.
Mbali na kumhoji meneja huyo, inadaiwa pia walifanya mahojiano na uongozi wa kiwanda kimoja kinachodaiwa kukutwa na vibali bandia vya wageni 84.
Taarifa hizo zilidai kuwa maofisa wengine waandamizi wa Uhamiaji kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam walitarajiwa kuwasili Moshi juzi kuungana na wenzao.
Baadhi ya maofisa waliotajwa katika ripoti hiyo kwamba wana utajiri ni wale waliokumbwa na uhamisho katika idara hiyo, Kia miezi mitatu iliyopita.
Katika ripoti hiyo, kigogo mmoja mwenye cheo cha DCI anadaiwa kukutwa na Sh700 milioni katika akaunti yake, achilia mbali kumiliki mali za mamilioni.
Mbali na maofisa hao kumiliki mamilioni ya fedha taslimu, pia wanadaiwa ‘kufanya kufuru’ ya kununua magari ya kifahari, nyumba na viwanja.
Ripoti hiyo inayodaiwa kuandikwa na Maofisa Uhamiaji wazalendo, imepinga hatua ya kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine, maofisa wanaotuhumiwa kukutwa na utajiri ambao haulingani na vipato vyao.
“Tunataka ufanyike ukaguzi wa kina wa vibali vyote vilivyotolewa kati ya 2009/2010, 2010/2011 hadi 2012 na taasisi zote zionyeshe nakala za vibali,” imedai.
Pia taarifa hiyo imependekeza wenzao wote wanaotuhumiwa kuwa na utajiri wa kutisha wachunguzwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
“Haikuwa sahihi kuwahamisha na kuishia hapo, walipaswa wapelekwe Takukuru wachunguzwe chanzo cha utajiri wao.”
Pia wametaka kigogo anayemiliki akaunti ya Dola, achunguzwe ili kujua alikuwa akifanya biashara gani nje ya utumishi wa umma na kama alilipa kodi kiasi gani.
Baadhi ya maofisa Uhamiaji wamependekeza kusimamishwa kazi kwa kigogo huyo katika kipindi hiki kwa hofu ya kuingilia na kuvuruga uchunguzi.
Wiki iliyopita, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Magnus Ulungi aliwaambia waandishi wa habari kuwa imeundwa kwa tume ya kumchunguza kigogo huyo.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana jana zilisema tume hiyo imepanua wigo wa uchunguzi juu ya kuwapo kwa vibali bandia katika taasisi mbalimbali.
Kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Naodha alikaririwa akisema Kilimanjaro ni moja kati ya mikoa minane inayomtia kichefuchefu nchini.
Waziri huyo alisema baadhi ya watumishi wamekuwa wakijihusisha na mtandao wa uingiaji wahamiaji haramu nchini pia kutoa vibali bandia kwa wageni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipoulizwa juzi kuhusu sakata hilo alisema ni vyema Uhamiaji ikapewa nafasi ya kuchunguza suala hilo kwa kuwa tayari imeshateua tume ya uchunguzi.

“Kamishna Mkuu wa Uhamiaji tayari amelifanyia kazi jambo hilo kwa uzito unaostahili. Tuwape nafasi walichunguze si vyema kuanza kuingilia katika hatua hii ya mwanzo,” alisema.

Wahamiaji haramu
Serikali, bila mafanikio, imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kukomesha tatizo la wahamiaji haramu linalotajwa kuwa chanzo cha utajiri wa baadhi ya vigogo wa Idara ya Uhamiaji.
Miongoni mwa mikakati iliyowahi kutangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ni pamoja na idara hiyo kufanya utafiti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mzumbe kubaini chanzo cha ongezeko la wahamiaji haramu nchini.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake bungeni mwaka 2007/2008 , aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Joseph Mungai alisema matokeo ya utafiti huo ni kuisaidia Serikali kujua chanzo cha tatizo hilo na jinsi ya kupambana nalo kwa ufanisi zaidi.
Hatua nyingine zinazochukuliwa ni pamoja na maofisa Uhamiaji kushiriki katika vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya vijiji, ili kuwapa wananchi elimu juu ya masuala yanayohusu uraia na jinsi ya kukabiliana na wahamiaji haramu; Kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari; Kuweka mtandao wa kompyuta katika vituo vyote vya Uhamiaji ili kuviunganisha na makao makuu.

Pamoja na Serikali kutangaza mkakati huo miaka mitano iliyopita, wahamiaji haramu limeendelea kuwa tatizo sugu linalotia doa utendaji wa idara hiyo. HABARI KWA HISANI YA GAZETI MWANANCHI

Sunday, May 20, 2012

TASWIRA MKUTANO WA WANAYANGA:WAZEE WA YANGA WAMCHOMOA MWENYEKITI LOYD NCHUNGA MADARAKANI


Mwenyekiti wa Kamati ya Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali akitangaza kumfuta Uenyekiti wa timu hiyo, Lyod Nchunga, baada ya kutimiza kolamu  ya wanachama mia tano na hamsini na sita na wajumbe nane kujiuzuru rasmi leo wakati wa mkutano wa wanachamauliofanyika kwenye klabu hiyo, Mtaa wa Jangwani naTwiga jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa Yanga wakishangilia tamko la kumg'oa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Lyod Nchunga
 Mashabiki wa Yanga ambao si wanachama, wakifuatilia mkutano wakiwa mbali
 Mmoja wa wanachama wa Yanga, anayeitwa Nyachia akionyesha kadi yake wakati wa kujisajili kuingia kwenye mkutano huo. 
Tofauti na vikao vingine vya Yanga ambavyo hufanyika katika ukumbi wa  jengo la Klabu hiyo, mkutano huu wa leo unafanyika kwenye Uwanja nje ya jengo.

Friday, May 18, 2012

TASWIRA ZA REDDS MISS HIGHER LEARNING DODOMA 2012 NDANI YA UKUMBI WA KILIMANI USIKU WA KUAMKIA LEO



Redds Miss Higher learning 2011 Jackline Kinabo (aliyekaa) ambae amemaliza muda wake akiwa tayari kumvalisha taji Mshindi wa Miss Redds Higher Learning 2012 katika ukumbi wa kilimani usiku wa kuamkia leo 
Mshindi wa Taji la Redds Miss Higher Learning Dodoma Mwaka 2012 Virginia Mokili (Katikakati) akiwa katika Picha ya Pamoja na Mshindi wa Pili wa Taji hilo Jenipher Mafuru (Wa Kwanza Kulia) na Mshindi wa tatu Lilian Maleo (Wa Kwanza Kushoto) mara baada ya Shindano Kumalizika
Washiriki walioshiriki Katika Shindano la Kumsaka Kimwana Wa Redds Elimu Ya Juu Kanda ya Dodoma wakiwa katika Picha Ya Pamoja Kabla warembo walioingia Tano Bora Kutajwa
Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Kumsaka Mlimbwende Wa Redds Elimu ya Juu Kanda ya Dodoma 2012 walipokua wakipita Jukwaani Kuonyesha Mavazi yao
 Jaji Mkuu wa Shindano la Kumsaka Mlimbwende wa Redds Elimu ya Juu Kanda ya Dodoma akisoma Majina ya Washiriki waliobahatika Kuingia Hatua ya Tano Bora
Warembo waliofanikiwa kuingia katika Hatua Ya Tano Bora wakiwa katika Picha ya Pamoja kama wanavyoonekana
Mmoja wa washiriki alipokua Akichagua swali tayari kwa kulijibu
 
Muuandaaji wa shindano la Redds Miss Higher Learning Dodoma 2012 Evans Exaud alipokua akiwakaribisha watazamaji na mashabiki katika Shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Kilimani Usiku wa Kuamkia leo
 Meza ya Majaji wakiwa makini na Zoezi zima la kutafuta Mshindi
Mdau wa Maswala ya Urembo Ester Zanghi Akiwa Makini kufuatilia shindano la Kumtafuta Mlimbwende wa Taji la Miss Higher Learning Dodoma 2012 katika ukumbi wa Kilimani
Msanii wa Kizazi Kipya Barnaba Akitoa Burudani katika shindano La Kumsaka Mlimbwende wa Redds Elimu ya Juu Kanda ya Dodoma 2012 katika Ukumbi wa Kilimani Usiku wa Kuamkia leo
Afisa Utamaduni Wa Manispaa ya  Dodoma Mh Kishosha akimkabidhi Zawadi Mshindi wa Kwanza wa Taji la Redds Miss Higher Learning Dodoma 2012 Virginia Mokiri Mara Baada ya Kuibuka Mshindi
Mshindi wa Pili wa Taji la Redds Miss Higher Learning Dodoma 2012 Jennipher Mafuru akipokea Zawadi zake Kutoka Kwa Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Dodoma Mh Kishosha Mara baada ya Kutangazwa Kuwa Mshindi Wa Pili
Mshindi wa tatu wa taji la Redds Miss Higher Learning Dodoma 2012 Lilian Maleo akipokea zawadi ya King'amuzi kutoka Kampuni ya Star Time huku anayemkabidhi ni Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Dodoma
Walimbwende walipokua wakitoa burudani kwa mashabiki na watazamaji waliokuja kushuhudia ni nani atakayeibuka kidedea na Kuwa Redds Miss Higher Learning Dodoma 2012 shindano lililofanyika Katika Ukumbi wa Kilimani 
 Mshindi wa Taji la Redds Miss Higher Learning Dodoma 2012 Virginia Mokiri akiwa katika Picha ya Pamoja na Mmiliki wa mtandao wa LUKAZA BLOG, Josephat Lukaza Mara baada ya Kutangazwa mshindi katika kinyanganyiro cha Kuwania Taji la Redds Miss Higher Learning 2012 huku LUKAZA BLOG ikiwa mmoja kati ya Wadhamini wa Shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Kilimani usiku wa Kuamkia leo
 Baadhi ya wwatazamaji waliojitokeza kushuhudia nani ataibuka mshindi wa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kilimani

wadau innocent lynn antony na muddy hella wakiwa na msanii Barnaba
Washiriki wote wa Kuwania Taji la Miss Higher Learning Dodoma 2012 wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadhamini wa shindano hilo lililofanyika Katika Ukumbi wa Kilimani huku Virginia Mokiri Kuibuka MShindi wa Taji hilo

Nafasi za Kazi mpya



PERSONAL SECRETARY - SOMANGA
Qualification: Holder of form IV/VI certificate with Diploma in secretarial or full secretarial certificate
Apply: Station Manager
SomangaGas plant Tanesco
Box  26 ,Kilwa
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   22, 2012

STOREMAN
Qualification: Tertiary qualifications,valid Tanzania driving license will be added advantage
Apply: buzrecruitment@barrick.com
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   20, 2012

SITE SERVICES MANAGER
Qualification: Diploma or degree in hotel Management or food & beverage or recognition experience in catering and Accomodation
Apply: buzrecruitment@barrick.com
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   20, 2012

COMMUNITY RELATIONS MANAGER
Qualification: Bachelor degree in socilogy,economics,community development regional planning
Apply: buzrecruitment@barrick.com
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   20, 2012

STORE KEEPER FOR - MOROGORO
Qualification: College Diploma on sales and/or marketing
Apply: Human Resources Manager Sao Hill Industry Limited
Box  4730 , Dar es Salaam
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   25, 2012

SALES OFFICER - DODOMA
Qualification: College Diploma on sales and/or marketing
Apply: Human Resources Manager Sao Hill Industry Limited
Box  4730 , Dar es Salaam
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   25, 2012

SALES OFFICER - MOROGORO
Qualification: College Diploma on sales and/or marketing
Apply: Human Resources Manager Sao Hill Industry Limited
Box  4730 , Dar es Salaam
Details:Daily News
May 08, 2012
Deadline:  May   25, 2012

YARD MANAGER - MOROGORO
Qualification: University Diploma om marketing or business administration
Apply: Human Resources Manager Sao Hill Industry Limited
Box  4730 , Dar es Salaam
Details:Daily News
May 08, 2012
Deadline:  May   25, 2012

QUALITY MANAGER
Qualification: Advanced diploma or degree in food technology,laboratories(BLS)from recognized University or College
Apply: Email ;
recruitmentpowerfoods@gmail.com
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   22, 2012

LOGISTIC/WAREHOUSE OFFICER
Qualification: A holder of Certificate of East Africa Customs, Clearing and freight forwading practices from TRA Tax Administration
Apply: Email ;
recruitmentpowerfoods@gmail.com
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   22, 2012

FINANCIAL COTROLLER
Qualification: Bachelor of Commerce degree Accounting or MBA in Finance with mandatory professional qualification in the Accounting profession CPA(T) or equivalent
Apply: email;
recruitmentpowerfoods@gmail.com
Details:Daily News May 08, 2012
Deadline:  May   22, 2012

PERSONAL ASSISTANT MANAGEMENT
Qualification: Advanced Secondary education and Diploma in Secretarial studies
Apply: The Human Resources
Manager, AccesBank 
Box  95061 ,Dar es salaam
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   23, 2012

BRANCH MANAGER - DAR ES SALAAM
Qualification: Degree in Finance,Accountancy, Economics or equivalent full professional qualification  in banking
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

TELEPHONE OPERATOR / RECEPTIONIST- UNGUJA
Qualification: National form IV Certificate in Division III plus a certificate in front  Office Management fro a recognized Institution
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

CREDIT OFFICER - UNGUJA
Qualification: University degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

CREDIT OFFICER - PEMBA
Qualification: University degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

AUDITOR - UNGUJA
Qualification: University degree or Advanced Diploma in Accountancy,Finance,Banking ,Business Adminsistration or Computer Science or equivalent qualification
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

FINANCE OFFICER- 2 POSTS (UNGUJA)
Qualification: Holder of degree or Advanced Diploma in Accountancy or equivalent qualifications
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

RISK AND COMPLIAANCE OFFICER - UNGUJA
Qualification: Degree in Banking, Finance,Accounting or Business Administration, from recognized University or Institution
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

CUSTOMER SERVICES OFFICER
(ISLAMIC BANKING) -DAR ES SALAAM
Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

CUSTOMER SERVICES OFFICER
 (  ISLAMIC BANKING) -  PEMBA
Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

LEGAL OFFICER  -  UNGUJA
Qualification: University degree in law with bias in Company and Commerical law
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

CUSTOMER SERVICES OFFICER -  UNGUJA
Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

BANK OPERATIONS OFFICER- UNGUJA
Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

TELLER -  3  POSITIONS -  PEMBA
Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

TELLER -  2  POSITIONS -  UNGUJA
Qualification: Degree in Banking, Commerce, or Economics, or Business Administration, or Advanced Diploma in Banking or equivalent
Apply: The Managing Director 
The Peolpe’s Bank of Zanzibar Ltd
Box  1173 ,Zanzibar
Details:Daily News May 11, 2012
Deadline:  May   25, 2012

DEPUTY CHIEF FINANCIAL OFFICER
Qualification: A holder of Master’s Degree either in Accounts, Finance,Economics,Public Finance or equivalent qualification
Apply: Managing Director National Development Corporation
Box  2669 ,Dar es Salaam
Details:Daily News May 04, 2012
Deadline:  June   05, 2012

DEPUTY CHIEF EXECUTIVE OFFICER
Qualification: Post Graduate degree in Engineering,(Mechanical Electrical,Civil process,mining or geology),Economics or business Administration
Apply: Managing Director National Development Corporation
Box  2669 ,Dar es Salaam
Details:Daily News May 04, 2012
Deadline:  June   05, 2012 .hisani ya gazeti mwananchi

Dawa kudhibiti VVU yaanza kutumika rasmi


 

MAMLAKA ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), imeidhinisha dawa ya Truvada kuwa tiba ya kuzuia kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).Dawa hiyo ambayo awali ilikuwa katika kundi la zile zinazotumiwa kwa ajili ya Kupunguza Makali ya VVU (ARV), imepandishwa chati wakati ambapo tayari ipo sokoni ikiuzwa kama moja ya ARV za kawaida.

Kwa mujibu wa maelezo ya FDA, mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU bila kutumia kondomu na hatomuambikiza.

Matokeo ya utafiti huo yaliwahi kuchapishwa kwenye gazeti hili toleo la Februari 12, mwaka huu na sasa kilichofanyika ni FDA kuidhinisha Truvada ambayo ilionyesha kufanya kazi vizuri ikilinganishwa na ARV nyingine.

Uidhinishaji wa dawa
Jopo la wanasayansi 22 wa FDA waliokutana Jijini Washington wiki iliyopita, walipitisha Truvada baada ya kupitia ripoti ya utafiti kuhusiana na ufanyaji kazi wa dawa za ARV.

Wanasayansi hao waliisifu dawa hiyo baada ya kuonekana kufanya kazi vizuri kwa watu waliopo kwenye hatari ya kuambukizana VVU kwa kasi zaidi.

Kwa namna dawa hiyo inavyofanya kazi, mwathirika akiitumia hawezi tena kumwambukiza mtu mwingine ambaye atashiriki naye tendo la ndoa bila kutumia kondomu.

Lakini, dawa hiyo masharti yake hayatofautiani na yale ya ARV kwani mtumiaji atapaswa kuitumia maisha yake yote ili kumwekea kinga asiwaambukize wengine na yeye aishi muda mrefu.

Kulingana na ripoti ya utafiti uliofanyika Marekani, dawa hiyo ina uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU hadi asilimia 90.Hata hivyo, kwa watu ambao wamekuwa wakitumia dawa holela hasa za ARV, hali imekuwa tofauti kwani Truvada imeonekana ikifanya kazi kwa kiwango cha asilimia 44 tu.

"Hii ni ishara kwamba kuna kundi la watu ambao dawa hiyo haitafanya kazi kikamilifu kutokana na mazingira ya matumizi ya dawa holela,"ilisema sehemu ya ripoti.

Hata hivyo, wanasayansi wanasema  tatizo hilo linafanyiwa uchunguzi ili kupata njia bora ya kukabiliana na tatizo hilo.

Faida ya Truvada
Wataalamu wameeleza kwamba itasaidia watu ambao wana VVU lakini, hawapendi kufanya tendo la ndoa kwa kutumia kondomu."Leo ni siku ya tukio la kuwasisimua wengi katika kuzuia maambukizi ya HIV,” alisema mmoja wa wataalamu kutoka Taasisi ya kujitolea kusaidia jamii ya Fenway, Dk Kenneth Mayer ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa FDA walioipitisha dawa hiyo.

"Ingawa (Truvada) haikuweza kuonyesha uwezo wa asilimia 100 kuzuia maambukizi ya VVU, namna inavyofanya kazi itakuwa na matokeo mazuri ya kupambana na Ukimwi duniani,” alisema Dk Mayer.

Tahadhari
Hata hivyo, wataalamu hao walihimiza kuwepo kwa uchunguzi zaidi wa kitafiti ili kujua kama Truvada itafanya kazi vizuri duniani kote.Mtaalamu wa Dawa kutoka Taasisi ya Taifa ya Saratani nchini Marekani (NCI),  Dk Lauren Wood alilalamika akisema kuwa utafiti huo haukuzingatia matatizo ya figo.

Alisema matatizo ya figo yamekuwa yakijitokeza kwa waathirika wengi wa Ukimwi hasa barani Afrika."Mimi sikufurahishwa sana kwa sababu utafiti huu haukuzingatia maeneo ambayo watu wengi wako kwenye hatari ya maambukizi,” alisema Dk Wood.

Lakini, alisema utafiti uliofanyika nchini Marekani umeonyesha wazi kwamba ni dawa inayoweza kupunguza kwa kiwango kikubwa kasi ya kusambaa kwa VVU.

Wataalamu kadha nao walisema pamoja na Truvada kupitishwa na FDA, ni lazima maelezo ya kitaalamu yatolewe kwa madaktari ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi yake.

Mabingwa hao walipendekeza kwamba, wanaotumia kabla ya kuruhusiwa kutembea na wenzi wao bila kondomu lazima wachunguzwe kitaalamu ili wajulikane kama dawa iyo imewakubali au la.

Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Afya cha Cincinnati, Dk Judith Feinberg alikosoa ripoti ya uchunguzi akisema ilipaswa kwenda mbali zaidi katika kuchunguza madhara yanayoweza kujitokeza kwenye matumizi ya dawa hiyo.“Tusipokuwa makini katika hilo, tunaweza tukawa tumepitisha jambo ambalo litasababisha madhara zaidi kuliko faida,” alionya Dk Feinberg.


Utafiti wa ARV
Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins ni miongoni mwa wale ambao walifanya uchunguzi juu ya ARV, kuwa moja ya dawa zinazopunguza maambukizi ya VVU.

Watafiti hao walibainisha kuwa wale wanaotumia ARV baada ya muda fulani, huweza kushiriki tendo la ndoa bila ya kutumia kondomu na mtu ambaye hana VVU na asimwambukize kwa asilimia 95.

Mkuu wa Mtandao wa Maabara za Kuchunguza VVU katika chuo hicho, Profesa Susan Eshleman alisema kwenye ripoti ya ugunduzi huo, wamebaini dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa HIV, sasa zinaweza kutumika kama sehemu ya kuzuia maambukizi.

Profesa Eshleman alisema kwamba, mwathirika wa VVU anayetumia ARV kikamilifu, anaweza kujamiiana na mtu ambaye hana virusi bila kondomu na asimwambukize.

“Huu ni ugunduzi wa kustajabisha,” alisema Profesa Eshleman akifafanua: “Matokeo haya yameleta mapambazuko mapya katika sayansi ya kuzuia maambukizi na inawaweka watafiti kwenye mazingira mazuri zaidi ya kupata suluhisho la kukabiliana na maradhi haya.”

Walivyogundua
Profesa Eshleman anasema utafiti huo walioupa jina la HPTN 052, walifanya kupitia maeneo mbalimbali ya dunia.

Kwenye ripoti hiyo ambayo pia ilichapishwa kwenye jarida maarufu la kisayansi linaloitwa Science, watafiti hao walisema mtu anapotumia ARV, hufikia wakati fulani wingi wa virusi mwilini hupotea kiasi kwamba anakuwa karibu sawa na yule ambaye hajaambukizwa.

“Jambo la msingi katika utafiti huu ni kwamba dawa hizi za kurefusha maisha zinapotumiwa kikamilifu, hupunguza mzigo wa virusi mwilini kwa zaidi ya mara 200. Ni sawa na kusema inapunguza hadi kufikia karibu na sifuri,” inaeleza ripoti hiyo.

Ni katika mazingira hayo, ripoti hiyo inasema kuwa damu ya mwathirika inakuwa haina virusi na hivyo uwezekano wa kumuambukiza mpenzi wake unakuwa haupo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa ARV inafanya kazi mbili, kwanza kurefusha maisha ya mwathirika kwa kupunguza virusi mwilini na pili ni kumkinga asiambukize wengine.
Sifa nyingine ya ARV, alisema ni kupunguza uwezekano wa waathirika kupata ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kutokana na kiwango cha kinga za mwili kuongezeka.  HABARI KWA HISANI YA MCL

CHECK; TASWIRA HIZI HALAFU JIULIZE TUFANYE NINI KUJIKOMBOA NA UMASIKINI