Thursday, June 7, 2012

DILI HILO WADAU: Mamilioni kwa watakaowafichua al-shabaab

                                      
Serikali ya Marekani imetenga dola milioni 33 kwa watakaotoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa viongozi saba wa kundi la al-shabab nchini Somalia.

Marekani na wachambuzi wengine wa masuala ya usalama wamehusisha kundi hilo na lile la al Qaeda.
Viongozi hao ni pamoja na kiongozi mkuu zaidi Mohamed Abdi aw-Mohamed, maarufu Sheikh Mukhtar Abu Zubeyr au jina lingine Ina Gudane yaani mtoto wa Godane. Ndiye muasisi wa kundi hilo. Marekani itatoa dola milioni saba kwa atakayetoa taarifa za kupelekea kukamatwa kwake.
Pia katika orodha hiyo ni waanzilishi wengine, Ibrahim Haji Jama, au Ibrahim Afghani - kwa maana asili yake ni Afghanistan.

Fu'ad Mohamed Khalf jina lingine ni Shongole,huyu ni mfadhili wa kundi hilo. Amekuwa mmoja wa viongozi wa kuu katika kundi la zamani la mahakama za kiislamu lililoondolewa na wanajeshi wa Ethiopia mwaka 2006.
Bashir Mohamed Mohamud anasimamia shughuli za kijeshi za kundi hilo.
Kundi hilo linajumuisha msemaji wa zamani, Mukhtar Robow na mkuu wa ujasusi Zakariya Ismail Ahmed Hirsi.
Kundi la al-shabab tayari limepata shinikizo kutoka pande zote za nchi, huku vikosi vya Kenya na Somalia vikiendeleza mashambulizi kuelekea mji wa Kismaayo, mji wa mwisho ambao bado uko chini ya udhibiti wa Al-shabaab.

Huku kundi hilo likipoteza maeneo mengi , viongozi kama hao hawana budi ila kutafuta sehemu za kujificha.
Hapa watatafuta hifadhi miongoni mwa jamii ya wafugaji na wakazi. Na kwa pesa nyingi zilizoahidiwa,mtu yoyote anaweza kuwasaliti

No comments:

Post a Comment