Tuesday, June 5, 2012

Picha Za Ule Mkutano Wa Baraza La Vijana Wa CCM Uliofanyika Mkoani Dodoma

 Ndugu Ridhwan J. Kikwete akichangia jambo juu ya taarifa ya mapendekezo ya kamati ya Uboreshaji wa Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM)
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho na Uimarishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Hussein Bashe akiwasilisha Taarifa ya Mapendekezo ya kamati yake.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Martin Shigela, akielezea jambo juu ya mapendekezo ya Kamati ya maboresho.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Benno Malisa, akifafanua jambo katika kikao hicho.
 Naibu Katibu Mkuu (bara) wa  Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) akifafanua jambo katika kikao hicho cha kujadili maboresho ya umoja huo.
Wajumbe wakifuatilia taarifa ya kamati kwa umakini.
---
Vikao hivyo ambavyo vilianza rasmi tarehe moja June 1, 2012. ambapo hoja mbalimbali zimekuwa zikijadiliwa kwa kina, ambapo vikao vilivyotangulia vimejadili juu ya hoja ya Katiba Mpya na suala la Muungano wa Serikali ya Jamhuri ya Muun gano wa Tanzania. Ambapo wajumbe walichangia hoja mbalimbali za msingi kwa kuzingatia hali ya sasa ya siasa nchini na matukio sambamba na hoja hiyo, kama vile mijadala ndani ya majukwaa mbalimbali juu ya muundo wa Katiba ya sasa, mapungufu yake na mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya na pia mijadala juu ya maboresho ya Muungano.

Pamoja na hayo, kikao kiliadili juu ya mapendekezo ya jinsi ya kuimarisha na  kuboresho Umoja huo wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mapendekezo hayo juu ya jinsi ya kuboresho umoja huo yametolewa na Kamati maalum ambayo ilipewa jukumu la kupendekeza namna ya kuiboresha UVCCM katika kikao cha Baraza hili kilichokaliwa mnamo tarehe 19/03/2011, ili iweze kukidhi mahitaji ya Siasa za ushindani wa sasa na baadae.

No comments:

Post a Comment