Tuesday, June 19, 2012

Jeshi la Misri lajilimbikizia madaraka

Baraza la kijeshi linalotawala limetangaza amri ya kijilimbikizia madaraka huku nchi hiyo ikisuibiri matokeo ya uchaguzi wa urais.
Mwenyekiti wa baraza la kijeshi ,Hussein Tantawi
Stakatadhi kutoka kwa baraza kuu la kijeshi linasema kuwa uchaguzi mkuu mpya hauwezi kuandaliwa hadi kuwe na katiba mpya.
Kutokana na amri hiyo, sasa baraza hilo la kijeshi linachukuwa mamlaka ya mbunge.
Wakati huo huo chama cha Muslim Brotherhood kimetangaza kuwa mgombezi wake Mohammed Mursi, ndie mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanywa siku ya jumapili.
Bwana Mursi, anashindana na Ahmed Shafiq, ambaye alikuwa waziri mkuu wa mwisho katika serikali ya Hosni Mubarak.
Chama hicho cha Muslim Brotherhood kimesema kwamba baada ya kura zote kuhesabiwa mgombezi wao anashikilia uongozi wa kati ya 52%-48% dhidi ya Bwana Shafiq.
Kituo cha Televisheni kinachounga mkono chama cha Muslim Brotherhood kimetangaza kuwa Bwana Mursi amepokea kura zaidi ya milioni 13. Nacho kituo cha televisheni cha kitaifa kimetangaza kwamba anaongoza katika kura hizo.
Akihutubu katika makao makuu ya chama chao ,Bwana Mursi ameahidi kuwa atakuwa rais wa Wa-misri wote na kwamba hatalipiza kisasi.
Lakini wasimamizi wa kampeni za Bwana Shafiq wamepuuza tangazo linalodai kuwa Bwana Mursi ndie mshindi wa uchaguzi wa siku ya jumapili.


No comments:

Post a Comment