Wednesday, June 6, 2012

CHECK:NAPE AIPONDA OPERESHENI YA CHADEMA 'VUA GAMBA VAA GWANDA'

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye  akimbeba mtoto  Goodluck John wa shule ya awali ya Lutheran, iliyopo Melizine nje kidogo ya mji wa Njombe, baada ya kumkuta mtoto huyo akiwa na wanafunzi wenzake miongoni mwa watu waliokuwa wakisubiri msafara wa wake kupita eneo hilo akiwa njiani kuingia mjini Njombe.
--
.Asema waliowashauri kuibuni wamewaingiza 'mkenge'
.'Movement for Change' yao nayo ni ya kuchangisha fedha si kuleta mageuzi
.Asema itawachukua miaka mingi kuwa chama cha kweli cha siasa
--

NA BASHIR NKOROMO, NJOMBE

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye amewananga CHADEMA kwamba aliyewapa wazo la kuanzisha kauli mbiu ya 'Vua gamba vaa gwanda' amewaingiza 'mkenge'.

Alisema, Chadema wameingizwa mkenge kwa kuwa inajulikana wazi kuwa kaulimbiu hiyo ililianzishwa na CCM,  kukisafisha chama kiondokane na mafisadi wa aina zote, na kwamba kwa Chadema kuanzisha 'vua gamba vaa gwanda' maana yake wanafanya kampeni ya kubembeleza watu wa aina hiyo wasiotakiwa CCM na Tanzania kwa jumla wahamie kwao.

Nape alisema hayo, jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mlangali, wilaya ya Ludewa mko mpya wa Njombe, akiwa katika ziara ya kikazi katika mikoa mbalimbali kuimarisha uhai wa chama.

"Itakumbukwa, CCM kwa kuwa ni chama halisi cha siasa kwa kutimiza sifa, kinaendelea na mageuzi makubwa ya ndani, yanayoitwa 'Kujivua Gamba', ikiwataka wale wote wanaojihusisha na ufisadi wa ina zote kuondoka ndani ya Chama. Lakini Chadema kwa kujua au kwa bahati mbaya wameamua kupotosha maana halisi iliyo wazi ya zoezi hili kwa kuanzisha operesheni eti ya 'Vua Gamba, Vaa Gwanda'", alisema Nape na kuhoji;

"Je, kwa maana hiyo Chadema kama wamedhamiria hivyo na siyo bahati mbaya, wamemua kuutangazia umma wa Watanzania na dunia nzima kwamba wako tayari kuwapa hifadhi mafisadi wa aina zote ambao ni tishio kwa ustawi wa taifa letu la Tanzania, ili mradi tu wapate idadi kubwa ya wanachama?".

Nape alisema, kama Chadema wangetumia busara wangeanzisha operesheni 'Vua Gamba vaa Uzalendo', kwa sababu hakuna ambaye angeshangaa, kwa kuwa kinachosababisha watu kuwa mafisadi ni kutokana na kukosa uzalendo ndani ya mioyo yao.

"Kumwambia mtu avue nguo ya ina moja avae nguo ya rangi nyingine huo ni upuuzi, maana aina ya nguo inaweza kuwa utambulisho tu, lakini haisaidii kubadili wala kujenga tabia ya mtu kiasi cha kuachana na ufisadi akawa mwadilifu na mzalendo kwa nchi yale toka moyoni, mtu anaweza kuivaa na kuivua wakati wowote, lakini kama watu wakihimizwa kuvaa uzalendo  wakauvaa sawa sawa, watakuwa nao mioyoni mwao daima, na hawatauvua muda wowote kama nguo", alisema.

Nape alisema kutokana na hali hiyo Wana-CCM wadilifu wasiwe na wasi wasi kuhusu 'magamba' yanayohamia Chadema, kwa sababu kwa kujiingiza katika kuyaona 'magamba' ambayo yamekubuhu kwa ufisadi kuwa ni mtaji kwao sasa chama hicho kinajichimbia kaburi.

"Wewe umesafiri kwa muda mrefu na gari lako, ukaliona mwendo wake umeanza kuwa wa ndivyo sivyo, ukaamua kuondoa oil chafu kusafisha injini, sasa wakati unasafisha akatokea mtu kuikinga akidhani itamfaa, wewe una hasara gani? si unamuacha tu akahangaike nayo?, alisema Nape.

Katika mkutano huo ambao ulijaa watu licha ya kufanyika kijijini, Nape aliponda operesheni iliyoambana na 'vua gamba vaa gwanda' ya 'Momement for Change-M4C', akisema hiyo ni operesheni ya kukusanya fedha tu, wala siyo ya kuleta  mabadiliko kama Chadema wanavyodanganya watu.

Alisema, ni operesheni ya kutafuta fedha, na ndiyo maana kila wanapoitangaza operesheni hiyo, wanachangisha watu fedha ambazo baadaye huwa wachangishwaji hawaambiwi ni fedha kiasi gani kimepatikana.

"Ukinunua kitu ukahitaji fedha iliyobaki si unasema nipatie 'chenji' yangu? sasa wananchi muwe macho, msidhani hiyo ni operesheni ya mabadiliko, ni operesheni ya wanaharakati kutafuta fedha, maana hata wao walishakiri kwamba Chadema ni chama cha harakati na sasa kinajaribu kujitoa kwenye uana harakati kiwe chama cha siasa cha kutafuta kutawala nchi" alisema na kuongeza;

"Lakini nawahaapia, hawa watakuwa wanaharakati kwa muda mrefu sana, itawachulua muda mrefu kuwa chama cha siasa kwa kuwa historia inathibitisha kuwa makundi mengi ya harakati yalichukua miaka mingi sana ndipo yakawa vyama vya ssembuse hawa,watakula fedha zenu mpaka mtachoka", alisema Nape.

Nape jana alitarajiwa kufanyika mikutano mingine ya hadhara katika mkoa wa Njombe kabla ya kujerea Dar es Salaam kwenye maandalizi ya mkutano mkubwa wa CCM wa wajumbe wa mashina, matawi na viongozi mbalimbali wa CCM na wanachama, utakaofanyika kwenye viwanjan vya Jangwani, Juni 9, 2012.

No comments:

Post a Comment