Mwenyekiti
wa Wabunge wa Tanzania EALA, Alhaji. Adam Kimbisa akinon'goneza Katibu
wake Shy-Rose Banji jambo wakati wa ufunguzi wa tafrija yao.
'Kaka wa Taifa' Makongoro Nyerere akitoa neno la shukrani kwa wageni wote waliohudhuria hapo. Pamoja nae ni Dkt Twaha Issa Taslima
Awali mama Maria Nyerere alihudhuria sherehe za Kuapishwa Wabunge hao
ambapo Mtoto wake Charles Makongoro Nyerere nae aliapishwa kulitumikia
Bunge hilo.
Shy-Rose Banji akipongezwa na ndugu na jamaa zake.
Wabunge wakipongezana baada ya kiapo nje ya Ukumbi huo wa Bunge uliopo Jengo la AICC mjini Arusha
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimpongeza Shy Rose.
Picha ya marafiki na familia
'Kaka wa Taifa' Makongoro Nyerere
Abdula Mwinyi na Mkewe kati pamoja na Mbunge wa Bunge la Tanzania, Magige wakipata msosi
Waheshimiwa hawa nao walikuwepo...
Lady Jay Dee akifungua shampaing na kuwamiminia watu.
Wakati wa Chiiiiiiiizz!!
Wabunge
wa Bunge la Afrika Mashariki upande wa Tanzania jana usiku mara baada
ya sherehe za Kuapishwa na uzinduzi wa Bunge hilo jipya la tatu
walifanya sherehe ndogo ya kujipongeza iliyofanyika katika Hoteli ya
Kibo Palace ya mjini hapa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwapo
ndugu jamaa na marafiki.
No comments:
Post a Comment