Thursday, May 17, 2012

WACHEZAJI WAMLILIA MCHEZAJI MWENZAO MAREHEMU PATRICK MAFISANGO ALIYEKUFA KWA AJALI USIKU WA KUAMKIA LEO




 Mkurugenzi wa mtandao wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku kulia akimsikiliza Katibu Mkuu wa timu ya Simba Bw. Evodius Mtawala wakati alipokuwa akielezea mipango ya kuuhifadhi na kuusafirisha mwili wa mchezaji wao marehemu Patrck Mafisango Mutesa aliyeafiki alfajiri ya usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chang'ombe Veta jijini Dar es salaam,  wakati akirejea nyumbani kwake na kusababisha watu wengine aliokuwa nao kupata majeraha.



Bw. Mtawala amesema hayo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kueleza kwamba kwa sasa wanawasiliana na Ubalozi wa Rwanda na mashirika ya ndege ili kukamilisha utaratibu wa vibali mbalimbali tayari kwa kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda nchini Rwanda kwa mazishi na taarifa kamili ya lini utasafirishwa itatolewa kesho mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote, katika picha kushoto ni Bw. Mwakitalima  mmoja wa mashabiki wa Simba aliyefika muhimbili kushuhudia kilichotokea.


 Mchezaji wa timu ya Simba Haruna Moshi Boban akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na jamaa na marafiki baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji mwenzao marehemu  Patrick Mafisango katika hospitali ya taifa ya Muhimbili .


 Wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga kushoto na Uhuru Selemani wa Simba wakisikitika wasijue la kufanya baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji mwenzao marehemu Patrick Mafisango  katika chumba cha kuhifadhia maiti muhimbili leo.


 Mbunge wa jimbo la Korogwe CCM Steven Ngonyani Prof Maji  Marefu akizungumza na wanahabari hospitalini hapo kuelezea masikitiko yake juu ya kifo cha mchezaji huyo.


 Haruna Moshi akitoka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti huku akilia kwa uchungu baada ya kuhakikisha kweli mwenzao Patrick Mafisango amefariki.


 Hapa Haruna Moshi akihojiwa alijaribu kuongea lakini akashindwa.


 Mchezaji Uhuru Selemani akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na mmoja wa waombolezaji.


 H


 Mchezaji wa zamani wa Simba Boniface Pawasa akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na Mchezaji haruna Niyonzima wa Yanga, Pawasa amesema jana walikuwa naye kwenye muziki katika klabu ya Maisha Oysterbay wakati bendi ya Akudo Impact ikifanya onyesho klabuni hapo na marehemu alimuaga kwamba anaenda nyumbani baadae akapigiwa simu kwa simu ya marehemu akiambiwa mwenye simu hii amefariki dunia kwa ajali.


 Boniface Pawasa kushoto, Uhuru Selemani wakilia.


 Uhuru Selemani akisalimiana na wanamuziki wa bendi ya Akudo Impact ambao pia wameelezaea masikitiko yao kwani wamesema marehemu walikuwa naye usiku wa kuamkia leo katika klabu ya Maisha ambako walikuwa wakifanya onyesho lao.


 Aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Simba Mrundi Ramadhana Wasso akihojiwa na waandishi wa habari kuelezea masikitiko yake kutokana na msiba huo.


 Mashabiki wa Simba wakiwa katika hospitali ya Muhimbili kwa masikitiko makubwa kwa kuondokewa na mchezaji wao kipenzi.


Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment