Thursday, April 19, 2012

CHELSEA YAILIZA BARCELONA


                              
 Didier Drogba akifunga goli
 
Goli moja la Didier Drogba la dakika ya 45 lilitosha kuipatia ushindi timu ya Chelsea almaarufu kama The blues watoto wa Darajani jijini London. Mechi ilikuwa ngumu na ilitawaliwa kwa kiasi kikubwa na Barcelona kama ilivyo kawaida yao ya kupiga pasi nyingi na kuwaacha Chelsea kuwa wakabaji muda wote.
Jitihada za Barcelona kupata goli ziligonga mwamba kutokana na ubora wa safu ya ulinzi ya Chelsea ambayo ilikuwa haipitiki kiurahisi huku golikipa wao Peter Cech akiwa imara golini kuidaka michomo yote ya timu pinzani. Chelsea na Barcelona wanasubiri kurudiana tena kipindi kijacho katika uwanja wa nyumbani wa Barcelona wa Nou Camp.
 Drogba akishangilia mara baada ya kufunga goli
Vikosi
Chelsea (4-3-3): Cech; Ivanovic, Cahill,Terry (c), Cole; Lampard, Mikel, Meireles; Mata (Kalou 73), Drogba, Ramires (Bosingwa 86).
Wachezaji wa akiba wasiotumika: Turnbull, Essien, Malouda, Torres, Sturridge.
Mfungaji: Drogba  dk 45

Barcelona (4-3-3): Valdes; Alves, Puyol (c), Mascherano, Adriano; Xavi (Cuenca 85), Busquets, Iniesta; Messi, Sanchez (Pedro 65), Fabregas (Thiago 78).
Wachezaji wa akiba wasiotumika:: Pinto, Pique, Batra, Keita.
Refarii:  Felix Brych
Watazamaji:  
38,039

No comments:

Post a Comment