Monday, April 23, 2012

Sudan yashambulia kusini


Uharibu uliotokea kwenye kisima cha mafuta kwenye jimbo la Unity, Sudan Kusini
Juma lilopita, wanajeshi wa Sudan Kusini waliteka visima muhimu vya mafuta vya Sudan kaskazini, huko Heglig, na kuzusha malalamiko ya kimataifa na msukosuko mkubwa.
Na picha za satalaiti ya Marekani zinaonesha kuwa sehemu muhimu ya miundo mbinu kwenye visima hivo iliharibiwa vibaya.
Siku ya Ijumaa Wasudan Kusini waliondoka, au walitimuliwa kwa mujibu wa taarifa za Sudan.
Na huko kusini, miripuko kadha kwa mpigo ilisikika masafa ya maili kadha.
Sudan Kusini ilisema hilo lilikuwa jaribio la kuharibu mtambo wa kusafisha mafuta katika kisima cha mafuta kwenye jimbo la Unity.
Naibu wa mkuu wa idara ya usalama ya jeshi la Sudan Kusini, Jenerali Mac Paul, alisema kulitokea mapambano kidogo baina ya wanajeshi wake na wale wa Kaskazini, karibu na mpaka wenye utatanishi.
Haikuwezekana kupata taarifa ya jeshi la Sudan.
Lakini ni wazi kuwa Sudan Kusini ina wasiwasi kuwa itashambuliwa na Sudan.
Juma hili Rais Omar el Bashir amesema anataka "kuikomboa" Sudan Kusini kutoka "wadudu" wanaoingoza nchi hiyo.
Alikasirika baada ya Sudan Kusini kuviteka na kuvikalia kwa juma zima visima vya mafuta vya Heglig, chanzo cha pato kubwa kwa serikali ya Khartoum.
Makamo wa rais wa Sudan Kusini, Riek Machar, aliiambia BBC kwamba wanajeshi wake wako tayari kuiteka tena Heglig, iwapo watashambuliwa tena.

No comments:

Post a Comment