Sunday, April 15, 2012

MAANDAMANO MAKUBWA YAFANYIKA SYRIA

Maandamano makubwa yafanyika Syria  
Sunday, 15 April 2012

Damscus,
WATU watatu wameuawa  katika maandamano makubwa  nchini Syria yaliyoitishwa na wapinzani wa utawala wa Rais Bashar al-Assad hapo jana.
Kamati ya uratibu ya kundi la wapinzani ilieleza kwamba watu watatu waliuawa katika maandamano hayo  yaliyofanyika katika mikoa ya Daraa, Hasakeh na Hama.
Nalo shirika la kutetea haki za binadamu Syria lenye makao yake makuu mjini London, Uingereza, limeripoti kwamba maofisa wa usalama walitumia risasi kuwatanya watu waliokuwa wakiandamana.
Kulingana na taarifa za shirika hilo, maandamano yalifanyika katika mji wa Idlib ulioko kaskazini mwa Syria, katika vionga vya mji mkuu Damascus na pia katika miji ya Daraa, Homs na Latakia.
Mwenyekiti wa shirika hilo la kutetea haki za binadamu, Rami Abdul-Rahman, alisema kwamba kwa ujumla makubaliano ya kusitisha mapigano bado yanatekelezwa kwa sehemu kubwa, licha ya kwamba yanavunjwa kwa kiasi kidogo.
 Hata hivyo wanaharakati wanaeleza kwamba majeshi ya Assad yaliwakamata waasi kiholela katika mji wa Daraa katika jaribio la kuwafanya waasi hao watumie nguvu dhidi ya jeshi la Assad.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana  lilitarajiwa kupitisha uamuzi wa kupeleka waangalizi wa kimataifa nchini Syria. Wanadiplomasia walieleza kwamba kundi la waangalizi 20 hadi 30 huenda likapelekwa nchini humo mwanzoni mwa wiki ijayo.
Ahmad Fawzi, ambaye ni msemaji wa mjumbe maalum nchini Syria, Kofi Annan, aliwaambia waandishi wa habari kwamba kundi la wajumbe 10 hadi 12 liko tayari kwa ajili ya kutumwa kwenda Syria.
Kinachosubiriwa sasa ni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha kutumwa kwa wajumbe hao. Fawzi aliendelea kusema kuwa uamuzi wa kupeleka kundi la pili lenye hadi waangalizi 250 itabidi uainishwe pia na baraza la usalama.

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa alisema hakutarajia kwamba amani ingerejea Syria kwani alikuwa na wasiwasi juu ya nia ya rais Assad. Naye Kofi Annan ameitaka Syria sasa kufungua njia ili iweze kupelekewa misaada ya kibinadamu.
 Wakati huohuo Uturuki imeanza kupokea misaada kutoka nje kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi wapatao 25,000 walioingia nchini humo wakitokea Syria.

No comments:

Post a Comment