Wednesday, April 18, 2012

Mbunge wa Temeke(CCM)Abbas Mtemvu Apata Ajali Mkoani Morogoro





 Mbunge wa Temeke(CCM)Abbas Mtemvu
---
MBUNGE wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu, amepata ajali mkoani Morogoro, leo baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kugongana na lori.

Taarifa za ajali hiyo zilitangazwa na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai katika mkutano wa saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano linaloendelea mjini Dodoma.

Ndugai amewaambia wabunge kuwa taarifa hizo ameletewa na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Dar es Salaam, Idd Azzan, ambaye alidai kuwa amepigiwa simu na Mtemvu.

Naibu Spika , amewaambia wabunge kuwa hali ya Mtemvu na watu waliokuwemo kwenye gari hilo,wamenusurika, bali wamepata majeraha madogo madogo na kwamba watakapofika Dar es Salaam, watakwenda kupata tiba hospitalini.Inadaiwa ajali hiyo ilitokea leo saa 12 asubuhi.

No comments:

Post a Comment